Kucheka kuna umuhimu zaidi ya kufurahia kitendo chenyewe

watoto wakicheka Haki miliki ya picha Getty Images

Rais wa Marekani Donald Trump aliwachekesha watu mwezi Septemba mwaka jana alipowaambia wajumbe wa Umoja wa mataifa kuwa utawala wake umepata ufanisi zaidi ukilinganishwa na tawala za watangulizi wake katika historia ya nchi hiyo.

Bw. Trump alikiri kuwa hakutarajia watu wangelimcheka lakini alisema "hiyo ni sawa".

Huo ni mfano wa sababu nyingi zinazowafanya watu kucheka- na mara nyingi sio kwa kuwa mtu ni mcheshi.

Kicheko ni kiungo muhimu kinachowaleta watu pamoja; uwezekano wa mtu kucheka upo mara 30 zaidi akiwa na wenzake kuliko akiwa peke yake.

Sio wanadamu pekee wanaocheka, wanasayansi wamebaini kuwa hata baadhi ya wanyama wakiwemo sokwe mtu na hata panya hucheka.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanasayansi wanasema kuwa wanyama wa porini pia wanacheka

Kwanini tunacheka

Kicheko ni njia moja ya kujieleza, katika mawasiliano kama kupiga kelele au kulia.

Sauti tunayotua wakati tunapocheka ni sawa na sauti inayotolewa na masokwe wakati wanapocheza.

Tofauti na matamshi, sauti tunayotoa wakati tunapocheka inahusishwa na viungo vingine vya mwili kutofanya kazi kwa wakati huo.

Japo wanasayansi hawajabainisha sauti hiyo hutokana na nini wanasema huenda ni njia moja ya kutoa sauti bila kuhusisha matamshi.

Wachekeshaji wanakipawa maalum cha kuwafanya waatu kucheka lakini kuna wengine wengi ambao wanatumia kicheko chenyewe kuwafanya watu kucheka.

Viongozi pia wanashindwa kujizuia kucheka

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bill Clinton na Boris Yeltsin

Rias wa zamani wa Marekani Bill Clinton alipata umaarufu baada ya kutumia kicheko kuujiandaa kabla ya kutoa taarifa ya pamoja na waziri mkuu wa Israel Boris Yelsin wakati walipokua wanatoa taarifa ya pamoja.

Hata hivyo Bw Clinton alikuwa muangalifu asionekane kana kwamba anamchekea mwenzake, kuashiria kuwa wote walikua wanafanya mzaha.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia UN mwezi Septemba

Kicheko ni dawa

Kicheko sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku.

Kwa mfano ushawahi kumpiga kumbo mwenzako bila kukusudia mkajiapa wote mnacheka?

Wataalamu wanasema mnacheka kwa sababu kila mmoja weno anahisi hakuna aliyemkosea mwenzake.

Njia hii ya mawasiliano ilikuwa na ufanisi kwa sababu wahusika walitumia kicheko kuelewana.

Utafiti unaonesha kuwa mara nyingi kicheko hutokana na kauli ya mtu au maoni sio lazima afanye mzaha.

Katika mazungumzo mtu anaecheka mara nyingi huwa anajibu kauli ya mtu bila kutumia maneno.

Kicheko kinaunganisha watu hali ambayo kila muda unavyosonga inadumisha ushirikiano wa kijamii.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Boris Johnson stuck alikwama kwenye waya wa chuma katika bustani ya Victoria Park

Utafiti wa hivi karibuni uliyofanywa kuhusiana na kicheko unaashiria kuwa watu wana uwezo wa kutumia vyema njia hii ya mawasiliano wanapotimia umri wa miaka 30 na kuendelea.

Pia unasema kuwa inategemea malezi ya mtu na umri wake; kwa mfano vijana waliyo na usumbufu wa kiakili huenda wasifurahie kucheka wakilinganishwa na vijana wenzao.

Jambo lingine muhimu ni kwamba kicheko husaidia mtu kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

Watu wanaojadiliana tofauti zao katika mahusiano kwa kutumia kicheko wanaweza kuelewa bila tatizo lolote.

" Jifunze kucheka unapokosea, na jaribu kuona mambo kwa njia nzuri hata wakati hali inapokuwa ngumu."

Hatahivyo hilo litafanikiwa ikiwa wote watafurahia kutaniana hata wakati wamekosana kido kwani hilo ni jambo la kawaida.

Wapenzi wanaotaniana hata wakati wanapopitia hali ngumu whuishi pamoja kwa muda mrefu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii