Tetesi za soka Ulaya Jumapili 27.01.2019: Hazard, hudson-Odoi, Morata, Malcom, Kompany, Bergwijn

Mshambuliaji wa Chelsea Eden hazard

Mshambuliaji wa, Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 28, ananyatiwa na klabu ya Real Madrid baada ya mabingwa hao wa kombe la vilabu bingwa Ulaya kusema kuwa wamesitisha mipango yao ya kumsaini kiungo wa kati wa Denmark 26, Christian Eriksen kutoka Tottenham..(AS)

Klabu ya Bayern Munich inatarajiwa kuwasilisha ombi la £40m kumununua mchezaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, huku klabu ya RB Leipzig ikiwa pia inammezea mate kinda huyo wa timu ya Uingereza isiozidi miaka 19. (Mail on Sunday)

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 26, atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu na Atletico Madrd siku ya Jumapili kabla ya mchezaji huyo wa Uhispania kukamilisha uhamisho wake wa mkopo.(Sky Sports)

Manchester United wameitaka klabu ya Uhoplanzi ya PSV Eindhoven kuwaelezea kuhusu mipango yoyote ya kutaka kumuuza winga wa Uholanzi Steven Bergwijn baada ya Bayern Munich kujiunga katika harakati za kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.. (Sunday Mirror)

Arsenal wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Malcom, 21, na wanatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kabla ya Alhamisi ambayo ndio siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho . (Sun on Sunday)

Manchester United haitafanya uamuzi wa haraka kumsajili mkufunzi mpya, licha ya Ole Gunnar Solskjaer kushinda mechi nane mfululizo tangu alipochukua uongozi wa klabu hiyo.(Sunday Mirror)

Crystal Palace inamtaka kwa mkopo beki wa Chelsea mwenye umri wa miaka 33 Gary Cahill, ikimaanisha kwamba mchezaji mwenza wa Uingereza beki Scott Dann, 31, huenda akajiunga na Fulham . (Sun on Sunday)

Southampton inafikiria kuwasilisha ombi la kumsajili nahodha wa klabu ya Uskochi ya Rangers James Tavernier, 27, lakini mkufunzi wake Steven Gerrard anataka £8m ili kumwachilia beki huyo wa Uingereza.. (Express)

Newcastle United iko tayari kuimarisha hamu yao ya kumsajili beki wa kushoto wa Monaco na Itali Antonio Barreca, 23. (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images

Hamu ya beki wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany ya kutia kandarasi mpya katika klabu hiyo inahatarishwa na hali ya maungo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32.(Sunday Mirror)

Kipa wa Liverpool na Brazil Alisson, 26, ametanagaza kwamba yeye na mkewe Natalia wanatarajia mtoto wao wa pili . (Instagram)

Klabu ya Monaco imemfuta kazi mkurugenzi wa kiufundi wa klabu hiyo Michael Emenalo kutoka katika jukumu lake la mkurugenzi wa michezo siku moja baada ya aliyekuwa mkufunzi Thierry Henry kupigwa kalamu na klabu hiyo.. (Mail on Sunday)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii