Sportpesa: Kariobangi Sharks 1- 0 Bandari

Wachezaji wa Kariobangi Sharks wakisherekea ushindi wao Haki miliki ya picha Sportpesa

Harrison Mwendwa ndio aliyekuwa mchezaji bora wa timu ya Kariobangi Sharks FC alipofunga bao la ushindi wa 1-0 dhidi ya Bandari fc kutoka Mombasa ana kuisaidia timu yake kushinda kombe la Sportpesa nchini Tanzania siku ya Jumapili.

Wakishiriki katika mchuano wao wa pili wa Sportpesa, Kariobangi Sharks ilionyesha mchezo wa hali ya juu na hivyobasi kufanikiwa kupanga tarehe na klabu ya Everton nchini Uingereza kwa ushindi huo uliowapatia USD30,000 pesa taslimu.

Timu hiyo ilioanzishwa miaka 2000 ilizidisha umaarufu wao katika mchezo huo baada ya kujiongezea kombe hilo huku wapinzani wao Bandari wakienda nyumbani na USD10,000 kufuatia hatua yao ya kufuzu katika fainali ya Jumapili.

Haki miliki ya picha Sportpesa

Kariobangi Sharks washinda kombe la Sportpesa Tanzania

Haki miliki ya picha Sportpesa
Haki miliki ya picha Sportpesa
Haki miliki ya picha Supersport
Haki miliki ya picha Sportpesa

Awali Mabingwa wa Tanzania Simba SC walikuwa na cha kujivunia baada ya kuchukua nafasi ya tatu katika kombe la Sportpesa 2019 walipowalaza wapinzani wao wa nyumbani Mbao FC kwa jumla ya magoli 5-4 kupitia mikwaju ya penalti siku ya Jumapili katikauwanja wa kitaifa mjini Dar es Salaam.

Mbao walinusurika mashambulizi makali kunako kipindi cha pili ili kulazimisha sare ya 0-0 kabla ya Simba ya Simba kupata ushindi huo katika michuano hiyo ya kila mwaka inayohusisha timu nane.

Haki miliki ya picha Picha/SPN

Ushindi huo uliipatia Simba kitita cha $7,500 pesa taslimu huku Mbao FC waliowatoa mabingwa mara mbli Gor Mahia wa Kenya wakijipatia $5,000 kwa kumaliza katika nafasi ya 4.

Siku ya Ijumaa timu za Kenya ziliiacha na kilio timu za nyumbani baada ya Simba na Mbao kupoteza mechi zao za nusu fainali dhidi ya Bandari FC na Kariobangi Sharks kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mbali na kulikosa taji hilo, timu hizo pia zimepoteza fursa ya kwenda Uingereza kucheza na klabu ya Everton ambayo itacheza na bingwa wa michuano hiyo.

Awali kabla ya Simba na Mbao kutolewa, ilionekana klabu za Tanzania mwaka huu zilikuwa na nafasi ya kulipa kisasi kwa Wakenya hasa baada ya timu kubwa za Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards kuondolewa katika hatua ya robo fainali.

Simba na Mbao zimewaangusha Watanzania baada ya kupoteza mechi hizo na kuwaachia wageni hao kutinga fainali.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii