Raia wa Zimbabwe wamzika gwiji wa muziki wa Afro-jazz Oliver Mtukudzi

Msafara wa a Jeneza la Mtukudzi ulipitia katika uwanja wa kitaifa wa michezo Haki miliki ya picha EPA
Image caption Msafara wa a Jeneza la Mtukudzi ulipitia katika uwanja wa kitaifa wa michezo

Waombolezaji walisafiri kote nchini Zimbabwe ili kuhudhuria mazishi ya mwanamuziki maarufu nchini humo Oliver Mtukudzi siku ya Jumapili.

Siku ya Jumamosi , jeneza lake lilizungushwa katika msafara kupitia uwanja wa kitaifa katika mji mkuu wa Harare.

Baadaye jeneza hilo lilisafirishwa na ndege aina ya helikopta hadi nyumbani kwao , kaskazini mwa mji mkuu wa Harare.

Msanii huyo ametoa albamu 67 na kuunda mwenyewe muziki wa mtindo wa Afro Jazz unaojulikana kwa jina marufu 'Tuku music'.

Mtukudzi alifariki Jumatano iliopita akiwa na umri wa miaka 66. Siku ya Alhamisi rais Emmerson Mnangagwa alimtangaza kuwa shujaa wa kitaifa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Msafara huo wa mazishi siku ya Jumamosi ulifuatiwa na tamasha la muziki kumuenzi mwenda zake

Alijipatia umaarufu wake 1970 akiwa mmojawapo wa sauti za uhuru zilizokuwa zikipigana dhidi ya wazungu walio wachache.

Nyimbo zake zilikuwa zikibeba ujumbe wa HIV/Aids pamoja na ile ya kisiasa.

Wimbo wake wa 'Wasakara' 2001, ukimaanisha ''You are too Old'' ulipigwa marufuku kwa kuwa ulionekana kumlenga kiongozi wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe , ambaye aliondolewa madarakani kwa nguvu miaka 16 baadaye akiwa na umri wa miaka 93.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii