Uteuzi wa Miss Rwanda wagubikwa na ukabila
Huwezi kusikiliza tena

Shindano la Miss Rwanda: Uteuzi wa Nimwiza Meghan wazua ukabila

Nimwiza Meghan ndiye msichana aliyeteuliwa kuwa Miss Rwanda mwaka 2019. Hata hivyo mchakato wa uteuzi wa Miss uligubikwa na kurushiana matamshi yenye ubaguzi wa kikabila baina ya wahutu na watutsi.

Baadhi ya wakereketwa wa makabila hayo walirushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii kila upande ukivutia kwake,hali iliyosababisha tume ya nchi hiyo ya kupambana na itikadi ya mauaji ya kimbari kutoa onyo kali kwa wanaochochea mgawanyiko wa kikabila chini ya kivuli cha kumteua Miss Rwanda.

Kutoka Kigali mwandishi wa BBC Yves Bucyana ametuma taarifa ifuatayo.