Wanafunzi wamuua mwalimu Kenya baada ya kuwapokonya simu

Ramani ya Kenya
Image caption Kenya

Wanafunzi watatu wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya mwalimu wao nchini Kenya baada ya kuwapokonya simu.

Peter Omari , mwalimu wa somo la Fizikia katika shule ya upili ya Hopewell mjini Nakuru, alishambuliwa siku ya Alhamisi.

Wanafunzi hawaruhusiwi kuingia shuleni na simu nchini Kenya kwa kuwa hulaumiwa kwa kuzitumia kufanya udanganyifu katika mitihani ya kitaifa mbali na swala la ukosefu wa nidhamu.

Uteuzi wa Miss Rwanda wazua ukabila

Tundu Lissu atamudu vishindo vya uchaguzi ndani ya Chadema?

Bata 'mpweke zaidi' duniani afariki

Maafisa wameambia BBC kwamba Omari amekuwa akisimamia masomo ya jioni.

Naibu kaunti kamishna wa eneo hilo Elim Shafi, alisema kuwa bwana Omari alikuwa anarudi nyumbani kwake ndani ya uwa wa shule hiyo yapata kilomita 150 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi wakati alipopigwa na kitu katika kichwa.

Mashambulio dhidi ya walimu pamoja na shule ni swala lililozua wasiwasi kwa mamlaka kulingana na mwandishi wa BBC Mercy Juma mjini Nairobi.

Mwaka uliopita, mwalimu aliuawa kwa kukatwa na panga na wanafunzi katika eneo la Kisume, Magharibi mwa Kenya baada ya mgogoro katika klabu moja ya burudani.

Mada zinazohusiana