Kuku wanaotaga mayai yalio na dawa ya kukabiliana na saratani

GM Haki miliki ya picha Norrie Russell, The Roslin Institute
Image caption Kuku hawa wana vinasaba vya mwanadamu vinavyoweza kuwasidia kutaga mayai yenye dawa muhimu

Watafiti wanamiliki kuku wenye vinasaba wanaotaga mayai yenye dawa inayoweza kukabiliana na saratani.

Dawa hiyo ni rahisi kutengeneza wakati watafiti hao wanapotumia mayai hayo ikilinganishwa na inapotengenezwa kiwandani.

Kuku hao huwekwa katika mazingira mazuri na hudekezwa ikilinganishwa na mifugo mingine, kulingana na Dkt Lissa Herron wa chuo cha kiteknolojia cha Edinburgh.

Kuku hao huishi katika eneo kubwa, hulishwa na kupewa maji na kuangaliwa na mafundi walio na ujuzi mkubwa , huku wakiishi maisha mazuri.

Kile wanachojua kuku hao ni kutaga mayai kama kawaida, haidhuru afya yao kwa vyovyote vile.

Wanasayansi hapo awali wameonyesha kwamba mbuzi wenye vinasaba, sungura na kuku wanaweza kutumiwa kutengeneza tiba ya protini katika maziwa yao na mayai.

Watafiti wanasema kuwa njia hiyo ina ufanisi mkubwa, inatoa mazao mazuri na haina gharama kubwa ikilinganishwa na majaribio ya hapo awali.

''Uzalishaji wa kuku ni rahisi mara 100 ikilinganishwa na ule wa viwandani. Hivyobasi tuna matumaini ya kupata gharama ya chini zaidi katika utengenezaji wa dawa hiyo kwa jumla'', alisema Dr Herron.

Haki miliki ya picha Norrie Russell, The Roslin Institute
Image caption Mayai haya yana dawa zilizotegenegezwa kwa bi ya chini zaidi

Gharama yake ni ya chini kwa sababu Ujenzi wa nyumba ya kuku ni wa bei nafuu ikilinganishwa na ule wa vyumba vidogo vya kuku ndani ya kiwanda.

Magonjwa mengi husababishwa na mwili wa binadamu kushindwa kutoa kiwango kidogo cha kemikali ama protini.

Magonjwa kama hayo yanaweza kudhibitiwa na dawa zilizo na protini hiyo. Dawa hizo hutengenezwa na kampuni za dawa na zinaweza kuwa ghali kutengeneza.

Dkt. Herron na wenzake walifanikiwa kupunguza gharama hiyo kwa kuweka jeni ya binadamu ambayo huzalisha protini hiyo katika mwili wa mwanadamu ndani ya vinasaba vya kuku vinavyohusika na kutengeneza weupe ndani yai la kuku.

Kiini cha yai

Baada ya kuvunja yai na kutenganisha weupe kutoka kwa kiini cha yai la kuku, Dkt. Herron aligundua kwamba kuku anamiliki protini hizo kwa kiwango cha juu.

Kundi hilo la watafiti limeangazia protini mbili ambazo ni muhimu katika kinga.

Ya kwanza ni ile yenye uwezo wa kukabiliana na virusi na athari za saratani na nyengine ni ile inayotenegenezwa kama tiba ya inayozifanya tishu zilizoharibika kujikarabati upya.

Mayai matatu yanatosha kutenegenza tiba na kuku wanaweza kutaga hadi mayai 300 kwa mwaka.

Wanasayansi hao sasa wanaamini kwamba wanaweza kutengeneza dawa nyingi za saratani ili kuuza iwapo kuku wengi watapatikana.

Utengenezaji wa tiba hiyo ya mwanadamu unaweza kuchukua takriban miaka 10 hadi 20.

Watafiti wana matumaini ya kutengeneza tiba ya wanyama wengine. Tiba hiyo itashirikisha dawa zitakazoimarisha kinga ya mifugo kama antibiotics , ambazo zitapunguza hatari ya magonjwa mengine yasiosikia dawa hizo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii