Je ni kweli kwamba wazazi wa watoto hao waliodaiwa kutekwa DR Congo wapo hai?

File pic of Congolese child in orphanage from 2018 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption DR Congo has Africa's biggest number of orphans, from war and outbreaks of disease (file pic)

Mamlaka nchini Ubelgiji imeomba kupewa sampuli za chembechembe za DNA za watoto waliodaiwa kuasiliwa kutoka DR Congo ili kubaini iwapo wazazi wao bado wapo wazima, kulingana na ripoti.

Wamewasiliana na wazazi wapya wa baadhi ya watoto 15 ili kubaini iwapo walitekwa nyara kulingana na magazeti ya Ubelgiji.

Viongozi wa mashtaka wanatuhumu kwamba wazazi wao walidhania kwamba walikuwa wakiwapeleka katika kambi moja ya likizo na sio katika nyumba ya mayatima nchini DRC .

Nyumba hiyo ya mayatima imefungwa.

''Wote wamepoteza katika tukio hili na jaji atalazimika kubaini ni wapi watoto hao watafaidika'', mbunge wa Flemish Lorin Parys aliambia BBC.

Je watoto hao walifanywa nini?

Maelfu ya watoto barani Afrika wameasiliwa katika miaka ya hivi karibuni kutoka mataifa ikiwemo Ethiopia na Uganda.

Hofu ya ulanguzi wa watoto nchini DR Congo ulililazimu taifa hilo la Afrika ya kati kusitisha vyeti vya kuruhusu kuasiliwa kwa watoto 2013.

Visa vingine vililazimika kuendelea kwa sababu tayari vililkuwa vimeanza.

DR Congo ina mojawapo ya viwango vya juu vya watoto mayatima , lakini iligunduliwa mwaka 201`7 kwamba watoto wanne ambao walikuwa wameasiliwa nchini Ubelgiji walikuwa wametangazwa kuwa mayatima kwa njia bandia.

Wote wanne walikuwa na kati ya umri wa miaka miwili na minne wakati walipopelekwa Ubelgiji kutoka nyumba ya mayatima ya tumaini mjini Kinshasa.

Kundi moja la waandishi wa Ubelgiji liliwatafuta wazazi wa watoto hao hadi katika kijiji kimoja kilichopo kilomita 850 kutoka mji mkuu wa Kinshasa.

Wazazi wao walisema kuwa watoto wao walikuwa wamepewa fursa ya kuondoka na shirika moja la vijana hadi katika kambi moja ya likizo lakini hawakurudi tena.

Kwa nini visa vipya vimejitokeza?

Tangu visa hivyo vipya kujitokeza , mamlaka ya Ubelgiji imechunguza msururu wa watoto kuasiliwa ambao walitoka katika nyumba ya mayatima ya Tumaini.

Wote 15 walidaiwa kuwasili nchini Ubelgiji kati ya mwaka 2013 na 2015.

Msemaji wa mwendesha mashtaka nchini Ubelgiji alisema kuwa wanandoa hao walizungumziwa kwa lengo la mtaalam wa vipimo vya DNA kwa watoto walioasiliwa, liliripoti Nieuwsblad.

Idara ya mahakama nchini Ubelgiji imepata ushahidi kwamba wazazi wa watoto hao ni wazima.

Kama wale watoto wengine wanne wazazi wao wanadaiwa kuwatuma watoto wao katika nyumba hiyo ya mayatima kwa madai kwamba walikuwa wakielekea katika kambi ya likizo.

Wakili wa Ubelgiji mwenye mizizi ya DR Congo Julienne Mpemba amechunguzwa kwa jukumu lake kama mkuu wa nyumba hiyo ya mayatima.

Wakili wake alikuwa hapatikani alipokuwa akitafutwa kutoa tamko siku ya Jumanne, hatahivyo awali ametangaza kuwa hahusiki kamwe.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii