Je michezo ya kamare inaleta hofu gani katika mataifa ya Afrika mashariki?
Huwezi kusikiliza tena

Kamari: Je mchezo huu unaleta hofu gani katika mataifa ya Afrika mashariki?

Michezo ya bahati nasibu kwa muda mrefu sasa imekuwa ikivutia wana Afrika Mashariki wengi, hasa makundi ya vijana.

Hata hivyo kasi ya vijana kujihusisha na michezo ya kubahatisha imeleta hofu kiasi cha baadhi ya serikali za nchi za Afrika Mashariki kupiga marufuku michezo hiyo.

Nchini Uganda hivi karibuni, Rais Yoweri Museveni alitangaza rasmi kuyafutilia mbali makampuni ya michezo ya kubashiri nchini humo.

Siku chache zilizopita Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ilizuia kwa muda urushaji wa matangazo ya michezo hiyo kupitia redio na televisheni, matangazo ambayo yalielezwa kukithiri.

Kutoka Dar es Salaam, mwandishi wa BBC Esther Namuhisa amezungumza na vijana wanaojihusisha na michezo ya kubahatisha:

Mada zinazohusiana