Upinzani Venezuela: 'Nimekutana na wanajeshi' asema kiongozi wa upinzani Juan Guaidó

Juan Guaidó Haki miliki ya picha AFP/Getty Images

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaidó amefanya mazungumzo ya siri na wanajeshi kutafuta uungwaji mkono wao wa kumng'atua madarakani rais Nicolás Maduro.

Mwezi uliyopita Bw. Guaidó alijitangaza kuwa rais katika hatua ambayo imeungwa mkono na Marekani na mataifa kadhaa ya Amerika kusini.

Mataifa ya Urusi na China yanamuunga mkono Maduro lakini msaada wa jeshi ni muhimu kwa juhudi zake za kusalia madarakani.

Mzozo ulianza baada ya Bw. Nicolás Maduro kuanza muhula wa pili madarakani licha ya uchaguzi kukumbwa na mzozo.

Wagombea wengi wa upinzani walizuiliwa kushiriki uchaguzi huo na wengine kufungwa jela.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro

Karibu watu milioni tatu wametoroka nchini Venezuela kufuatia mzozo wa kiuchumi huku taifa hilo likikumbwa upya na ghasia hivi karibuni.

Rais wa Marekani Donald Trump, siku ya Jumatano aliandika katika mtandao wake waTwitter kuwa amezungumza na Bw. Guaidó na kwamba anaunga mkono "Urais wake wa kihistoria", aliandika katika ujumbe wake wa pili kuwa "Harakati za kupigania uhuru zimeanza!"

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jeremy Hunt, anatarajiwa kuyashawishi mataifa ya Muungano wa Ulaya kuwaekea vikwazo maafisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Bw. Maduro leo Alhamisi baada ya kuzungumza na Bw. Guaidó siku ya Jumatano.

Guaidó aliandika makala katika gazeti la New York Time

"Tumefanya mkutano wa dharura na vikosi vya usalama," aliandika Bw. Guaido.

"Majeshi kuondoa msaada wao kwa Bw. Maduro ni sejemu muhimu sana katika harakati ya kuleta mageuzi serikalini na watu wengi wanaamini kuwa suluhisho la mzozo unaokumba nchi hii hauwezi kokomeshwa chini ya utawala huu."

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Maafisa wa usalama wa Venezuela

Makala hiyo pia inasema upinzani utatoa msamaha kwa maafisa wa usalama "watakaopatikana na hatia ya kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu".

Kama kiungozi wa bunge la nchi Bw. Guaidó anasema katiba inamruhusu kushikilia madaraka kwa muda wakati rais anapokiuka katiba.

Mahakama ya juu zaidi cnini Venezuela imemwekea marufuku kiongozi wa upinzani kutoondoka nchini na pia kupiga tanchi akaunti zake za benki.

Makala hayo ya Guaidó yanakuja siku kadhaa baada maandamano ya kumpinga Bw. Maduro kuanza.

Awali rais wa Venezuela Nicholas Maduro aliiambia shirika la habari la Urusi RIA kuwa anajianda kufanya mazungumzo na upinzani."kwa maslahi ya taifa zima la Venezuela".

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bw. Madura anatuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu

Aliongeza kuwa hayuko tayari kukubali vitisho au hujuma, na kusisitiza kuwa majeshi ya Venezuela yanamuunga mkono, huku akiwalaumu baadhi ya wanajeshi waasi kwa kupanga njama ya kupindua utawala wake.

Shinikizo la kidiplomasia

Viongozi wa Ulaya tayari wameonya ikiwa Bw. Maduro hatatangaza uchaguzi mpya kufikia Jumapili, wataungana na Marekani na mataifa mengine kumtambua rasmi kiongozi wa upinzani, Juan Guaido, kama rais wa mpito.

Siku ya Alhamisi, akihudhuria mkutano nchini Romania, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jeremy Hunt, alisema kuwa atawashinikizi wenzake barani Ulaya kutafakari uwezekano wa kuwaekea vikwazo washirika muhimu ndani ya serikali ya Bw. Maduro.

EU iliwaekea vikwazo viongozo 18 wa Venezuela kwa tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu na huenda orodha hiyo ikawashirikisha viongozi wengine zaidi.

Guaido, alizungumza na Bw. Hunt siku ya Jumatano na inadaiwa alitoa wito kwa muungano wa EU kuchukua hatua kali dhidi ya serikali mjini Caracas.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii