Wazee wengi nchini Japan ndio wanaotekeleza uhalifu wakitaka kwenda jela

Mfungwa nchini Japan

Japan inakabiliwa na wimbi la uhalifu unaokabiliwa na wazee - ambapo uhalifu unaotekelezwa na watu walio na zaidi ya umri wa miaka 65 umekuwa ukiongezeka kwa takriban miaka 20 sasa.

Katika nyumba moja mjini Hiroshima - kwa wahalifu wanaoachiliwa kutoka jela kurudi kwa jamii, Toshio Takata mwenye umri wa miaka 69 anasema kuwa alivunja sheria kwa sababu alikuwa masikini.

Alitaka kwenda mahali ambapo ataishi bila malipo, hata kama ni jela.

''Nilifikia umri wa pensheni na baadaye nikaishiwa na fedha''.

''Hivyobasi nilidhania kwamba pengine nitaishi bila kulipa chochote nikiwa jela'', anasema. 'Hivyobasi nilichukua baiskeli na kwenda hadi katika kituo cha polisi na kumwambia afisa aliyekuwepo ''tazama nilichukua hiki''.

Mpango huo ulifanikiwa .

Hayo yalikuwa makosa ya kwanza ya Toshio , akiyafanya akiwa na umri wa miaka 62 , lakini Japan inachukulia makosa hafifu kwa umuhimu mkubwa sana hivyobasi ilikuwa tosha kuhudumia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Akiwa mdogo, mwembamba, Toshio hakai kama muhalifu, na hafanani na mtu aliyemtishia na kisu mkewe.

Lakini baada ya kuachiliwa alipohudumia kifungo chake cha kwanza hiyo ndio hatua ya pili aliochukua.

''Nilienda nikawatishia na kisu nikisubiri kwamba mmoja wao atawaita maafisa wa polisi.. Mmoja wao aliwaita''.

Image caption Toshio aonyesha michoro yake ndani ya jela

Kwa jumla, Toshio amehudumu nusu ya miaka minane iliopita akiwa jela.

Nilimuuliza iwapo anapendelea kuwa jela- na ananielezea kuhusu ukosefu wa fedha -na pensheni yake inaenedelea kulipwa licha ya yeye kuwa jela.

''Sio eti napendelea lakini najua nitaishi huko bure'', anasema. ''Na ninapotoka najua kwamba kuna fedha nimewekewa. Hivyobasi sio uchungu''.

Toshio anawakilisha jamii inayoheshimu sana sheria, ambapo idadi kubwa ya uhalifu unatekelezwa na watu walio zaidi ya umri wa miaka 65 .

Mwaka 1997 , umri huu ulishirikisha takriban wafungwa 20 lakini miaka 20 baadaye takwimu hizo zilikuwa na kufikia mmoja kati ya wazee watano.

Image caption Idadi ya wazee wanaotekeleza uhalifu nchini Japan.

Na kama Toshio, wengi wa wazee hao wahalifu hurejelea makosa yao .Kati ya wazee 2500 walio na zaidi ya umri wa miaka 65 waliopatikana na uhalifu na kufungwa 2016, zaidi ya thuluthi moja ilikuwa na makosa matano hapo awali.

Mfano mwengine ni keiko{ sio jina lake }.

Ana umri wa miaka 70 , ni mdogo na aliyevaa nadhifu. Pia yeye anasema kuwa ni ufukara uliomsukuma kuchukua hatua hiyo.

''Sikuweza kuelewana na mume wangu . Nilikuwa sina mahala pengine pa kuishi. Hivyobasi ilikuwa chaguo langu kuiba'', anasema.

Hatahivyo wanawake walio na umri wa miaka 80 ambao hawawezi kutembea vizuri pia wanatekeleza uhalifu.

Ni kwa sababu hawawezi kupata chakula na fedha.

Tulizungumza miezi kadhaa iliopita. Nimeambiwa amekamatwa tena sasa anahudumia kifungo chengine jela kwa kuiba katika duka.


Wizi ni kitendo kikubwa cha uhalifu unatokelezwa na wazee hao.

Mara nyingi wao huiba chakula chenye thamani ya £20 katika duka wanalotembelea.

Katika gazeti lililochapishwa mwaka 2016, anahesabu kwamba gharama ya kukodisha nyumba , chakula na afya huwaacha wanahudumiwa madeni iwapo hawana kipato chengine.

Na hiyo ni kabla ya kulipia joto nyumbani na kununua nguo.

Hapo zamani ilikuwa utamaduni kwa watoto kuwaangalia wazazi wao .

Lakini ukosefu wa fursa za kiuchumi kumesababisha vijana kuondoka , na kuwawacha wazazi wao kujiangalia.

"Wazee hao hawataki kuwa mzigo kwa watoto wao na wanahisi kwamba iwapo fedha wanazopata kutoka kwa serikali hazitoshi basi wanaona kwamba njia pekee ya kuwanbdolea mzigo wanao ni kwenda jela.

''Kurejelea makosa ni mojawapo ya njia za kurudi jela ambapo kuna vyakula mara tatu, hakuna madeni'' , anasema.

Vilevile swala la wazee hao kujiua limeanza kuwa la kawaida ukiwa uamuzi mwengine ambao unawafanya kuhisi kwamba ni wakati wa kujiondoa duniani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii