Ni mataifa gani yanakula nyama zaidi duniani?

Wanawake wachoma nyama Haki miliki ya picha SOPA Images

Huenda umesikia watu kadhaa na pengine kwa idadi inayoongezeka wanaogeukia kula mboga za majani badala ya nyama.

Hii ni sehemu ya jitihada kwa baadhi kujaribu kuwana afya nzuri au kupunguza hatari ya kuugua magonjwa yatokanayo na kula nyama, kupunguza madhara kwa mazingira au kwa kujali tu maslahi ya wanyama.

Hali hii inatokana kwa kiwango fulani na jitihada zinazoshinikiza kula nyama kiasi na badala yake kula mboga kwa wingi.

Lakini je yana athari yoyote katika matumizi ya kila siku?

Kipato kinachoongezeka

Tunachokifahamu ni kwamba ulaji nyama duniani umeongezeka kwa kasi katika miaka 50 iliyopita.

Utengenezaji nyama leo ni karibu mara tano zaidi kiwango cha juu kuliko ilivyoshuhudiwa katika miaka ya 60. Kuanzia tani milioni 70 hadi zaidi ya tani 330 mwaka 2017.

Sababu kubwa ya hili ni kwamba kuna watu wengi zaidi wanaohitaji kula.

katika kipindi hicho, idadi ya watu duniani iliongezeka zaidi ya mara mbili.

Wakati idadi ya watu ni sehemu ya hadithi hii, haielezi kikamilifu kwanini utengenezaji nyama umeongezeka kwa karibu mara tano zaidi.

Jambo jingine muhimu ni kuongezeka kwa kipato.

Kote duniani, waut wametajirika, huku kipato cha wasani duniani kikiongezeka kwa mara tatu katika nusu karne.

Ukifanya ulinganifu wa ulaji kwenye nchi tofauti utaona kuwa kadri kipato kinavyokuwa na watu huzidisha kula nyama.

Si kuwa tu kuna watu duniani - lakini watu ambao wanaweza kununua na kula nyama.

Nani wanaokula nyama nyingi zaidi?

Mwaka 2013, ambao ndio mwaka wa hivi karibuni zaidi ambao taarifa zake aipo hadharani, nchi za Marekani na Australia waliongoza kwenye orodha ya ulaji wa nyama duniani pamoja na nchi za INew Zealand na Argentina.

Katika nchi hizo nne wastani ulikuwa mtu mmoja kula kilo 100 za nyama, sawa na kula kuku 50 au nusu ng'ombe kwa mwaka.

Hali ya ulaji wa juu wa nyama pia ipo katika eneo la Ulaya Magharibi ambapo wastani ni mtu mmoja kula baina ya kilo 80 na 90 za nyama kwa mwaka.

Nchi zote zenye wastani wa ulaji mkubwa wa nyama duniani ni tajiri.

Kwa upande wa pili, nchi masikini ndizo zenye wastani mdogo zaidi wa ulaji wa nyama duniani.

Rai wa kawaida nchini Ethiopia hula kilo 7 tu kwa mwaka, Mnyarwanda kilo 8 na Mnigeria kilo 9. Raia wa Ulaya hula nyama mara 10 zaidi ya wastani huu.

Kwa nchi masikini, nyama ni chakula cha anasa.

Nchi za uchumi wa kati zaja juu

Ni dhahiri kuwa nchi tajiri hula sana nyama, na nchi masikini hula kidogo.

Hali hiyo ipo kwa miaka 50 na zaidi sasa. Imekuwaje sasa ulaji wa nyama umekuwa duniani?

Mabadiliko makubwa yanachochewa na nchi za kipato cha kati ambazo uchumi wao umekuwa ukipanda siku hadi siku.

Nchi kama China na Brazil zimesajili mabadiliko makubwa chanya ya kiuchumi katika miongo ya hivi karibuni, na ulaji wao wa nyama umekuwa mkubwa pia.

Mtu wa kawaida nchini China kwa mwaka 1960 alikuwa akila chini ya kilo 5 za nyama kwa mwaka, mwishoni mwa miaka ya 80 ikapanda mpaka kufikia 20, na katika miaka ya hivi karibuni imepanda na kufikia kilo 60.

Hali kama hiyo imetokea pia nchini Brazil, ambapo ongezeko la kula nyama limepanda maradufu toka miaka ya 1990 na kupiku baadhi ya nchi za bara Ulaya.

Nchini Kenya pia ulaji wa nyama umebadilika sana toka mwaka 1960.

India hali ni tofauti kabisa.

Japo kipatu cha mtu mmoj mmoja kipaa mara tatu toka miaka ya 1990, ulaji wa nyama haujaongezeka.

Haki miliki ya picha PIUS UTOMI EKPEI

Na si kweli kuwa walio wengi nchini humo hawali nyama - ukweli ni kuwa theluthi mbili ya Wahindi hula aina fulani ya nyama, kuingana na matokeo ya sensa ya taifa hilo.

Hatahivyo, ulaji wa nyama nchini humo angali ni mdogo sana, kilo 4 kwa mwaka, wastani mdogo zaidi duniani. Hii ni kutokana na sababu za kiimani kutokana na baadhi ya watu kutokula aina fulani ya nyama kwa sababu za kidini.

Je ulaji wa nyama unaporomoka nchi za mgharibi?

Watu wengi barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini wanasema wanajaribu kupunguza ulaji wao wa nyama, lakini je hilo linafanikiwa?

Jibu ni hapana, kulingana na takwimu zilizopo.

Uhalisia ni kwamba ulaji wa nyama umeongezeka ktika miaka ya hivi karibuni nchini Marekani kwa mujibu wa wizara ya kilimo ya nchi hiyo (USDA)

Kwa mwaka 2018, ulaji wa nyama Marekani ulikuwa ni mkubwa zaidi kwa miaka ya hivi karibuni.

Hali ipo hivyo kwa nchi nyingi za Umoja wa Ulaya (EU).

Hata hivyo aina ya nyama inayoliwa ndiyo imekuwa na mabadiliko.

Ulaji wa ng'ombe na nguruwe unapunguwa kwa kasi, huku wa kuku ukipanda maradufu.

Kwa Marekani, ulaji wa kuku umefikia nusu ya ulaji wote wa nyama kwa sasa, toka robo tu katika miaka ya 1970.

Mabadiliko hayo ni habari njema kwa afya na mazingira.

Athari za nyama

Ulaji wa wastani wa nyama na maziwa una faida kwa afya ya binaadamu, hususani katika nchi za kipato cha chini ambapo chaguo la chakula huwa finyu.

Lakini katika nchi nyingi ulaji wa nyama unachupa mipaka ya faida za kiafya.

Ulaji mkubw na hovyo wa nyama unaweza sababisha hatari za kiafya mwilini.

Tafiti za kitabibu zinaonesha kuwa ulaji wa nyama kwa wingi hupelekea ongezeko la hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kiharusi na saratani.

Kubadilisha ulaji wa ng'ombe na nguruwe kwa kuku ni jambo bora zaidi kiafya.

Kwa utunzaji wa mazingira, ulaji wa kuku pia ni mzuri. Ufugaji wa ng'ombe huharibu mazingira mara 10 zaidi, nguruwe nusu yake.

Hali inavyoendelea ni kuwa, mabadiliko yapo kwenye aina gani ya nyama itaendelea kuliwa zaidi na kwa kiwango gani.

Lakini, jambo moja litaendelea kusalia pale pale, nyama ni mboga ya anasa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii