Kwa picha: Watu 2 wanaofanana na Rodrigo Duterte na Kim Jong-un wazua vioja Hong Kong

Impersonators Howard X (L) and Cresencio Extreme in Hong Kong, China, 3 February 2019 Haki miliki ya picha EPA

Huenda ukadhania kwamba rais wa Ufilipino Rodrigo Durtete na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walikuwa pamoja katika barabara za mji wa Hong Kong, wakipiga picha na kula pamoja chakula cha jioni katika mgahawa mmoja.

Lakini uchunguzi wa kina ulibaini kwamba wawili hao walikuwa watu waliowaiga viongozi hao wawili.

Kutana na jamaa anayejiita Cresencio Extreme anayefanana na Durtete na Howard X anayefanana na Kim Jong un.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wawili hao waliobeba bunduki bandia walisalimiwa na wafanyikazi na raia walipowasili katika mgahawa huo wa kuku karanga au Fried Chicken Restaurant
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Walihudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la St Joseph's huku Cresencio Extreme (kushoto)akiwa amevalia shati jeupe ambalo hupendwa sana na rais Durtete
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mtu huyo anayefanana na rais Durtete alizua kihoja na mkanganyiko katika kanisa hilo katikati ya mji wa Hong Kong baada ya kuzungukwa na waumini
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption "Je huyu ni Durtete?'' Wengine hawakukubaliana naye huku raia huyo akionekana kuwa mdogo kwa umri kuwa rais wa Ufilipino pamoja na mwenzake anayemuiga rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wawili hao walizidi kuwakanganya raia waliopoonekana wakila chakula cha jioni katika mgahawa wa Hong Kong siku ya Jumapili.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mr Duterte {kushoto) na muigaji wake
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bwana Kim (kushoto) na muigaji wake kulia

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii