Changamoto ya miundombinu yageuza kinyesi kuwa lulu Tanzania

MTAMBO

Katika makazi ya watu duni na maeneo yaliyojengwa kiholelala, moja ya changamoto kubwa ambazo watu hukumbana nazo ni namna ya kujenga miundombinu ya maji taka.

Nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania na Kenya zimekuwa zikichukua jitihada mabli mbali kutatua changamoto ya uhifadhi na uchakatwaji wa maji taka katika maeneo makaazi yasiyopimwa. Maeneo hayo kwa kiasi kikubwa hayawezi kufikiwa na magari ya kunyonya maji taka kutokana na ujenzi holela.

Jijini Dar es Salaam, kitongoji cha Mburahati ni moja ya maeneo ambayo kwa miaka kadhaa yamekuwa yakikumbwa na tatizo hilo, lakini kuna mradi kabambe unaochakata kinyesi cha binadamu na kutengeneza gesi ya kupikia chakula. Mtambo huo wa Mburahati unaweza pia kuchakata maji taka na kuyageuza maji safi na salama ya kunywa.

Mafanikio ya mradi huo, tayari yamewavuta wageni wanaotaka kujenga miradi kama hiyo katika nchi zao.

Hivi Karibui, mwandishi wa BBC Swahili Halima Nyanza aliambatana na maafisa kutoka Kenya ambao walitembelea mradi huo hivi karibuni ili kujifunza jinsi ya kujenga vyoo vya bei nafuu hususan katika maeneo yasiyo na mtandao wa maji na yaliyo duni.

Dokta Tim Ndezi, Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya CCI inayohusika na kujengea uwezo jamii katika masuala ya nyumba za bei nafuu, usafi wa mazingira, na alikuwa mmoja wa wenyeji wa ugeni huo.

"Wameweza kujifunza mambo mbalimbali si hapa mburahati tiu hata katika eneo la vingunguti ambapo wameona namna ambavyo nyumba zilizo kwenye makazi duni zinaweza kutirisha kinyesi katika mabwawa yaliyo karibu na makazi yao. Na wao wana mpango wa kujenga kitu kama kile katika eneo la Mkuru huko Nairobi," amesema Dkt. Kuna maeneo yao ambayo pia

Image caption Mtambo wa Mburahati una uwezo wa kuchakata maji taka na kuwa maji safi na salama ya kunywa

Eliwaza Kitundu ni mtaalamu katika mtambo wa kuchakata maji taka uliopo Mburahati barafu, "huu ni mfumo ambao unaweza tibu maji taka yaani kinyesi na kupata maji safi lakini pia tukapata gesi ya kupikia majumbani."

Lengo kubwa la miradi hiyo ni kuzuia maradhi ya mlipuko kama vile kipindupindo ambayo yamekuwa yakishamiri katika maeneo yenye mifumo duni ya udhibiti wa maji taka.

"Nimetoka Kampuni ya Maji Nairobi na kwa sasa tunatengeneza mpango kabambe wa maji taka katika eneo la Mkuru ambalo ni makazi duni. Pale kuna changamoto nyingi hususani wingi wa watu na ukosefu wa miundomsingi ya majitaka. Tumekuja hapa kujifunza nama ambavyo tunaweza pendekeza jinsi gani mradi wetu ujengwe kutokana na uzoefu wa hapa (Dar es Salaam)," amesema bwana James ambaye ni miongoni mwa wageni kutoka Kenya.

Image caption Changamoto kubwa ya ujenzi holela ni wakaazi wengi kutofikiwa na magari ya kunyonya maji taka na mwishowe hutirirsha uchafu huo na kuzua magonjwa ya mlipuko.

Wakaazi wa Mburahati pia wanamwagia sifa mradi huo ambao wanasema umechangia pakubwa kupambana na magonjwa ya mlipuko.

"Mburahati hii ilikuwa na changamoto kubwa sana ya magonjwa ya kipindupindu na kuhara, lakini sasa hali ni shwari, kinyesi kinashughulikwa ipasavyo," mkaazi wa Mburahati Venance Nunda ameiambia BBC.

Mada zinazohusiana