Je unajua sababu kwanini wanawake wanaishi maisha marefu zaidi ya wanaume?

Wanawake Africa Haki miliki ya picha YASUYOSHI CHIBA

Kote duniani, wanawake wanaishi maisha umri zaidi kuliko wanaume.

Kiwango cha wastani cha binaadamu duniani kuishi wanapozaliwa ni umri wa miaka 72 mnamo 2016, kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO).

Lakini wakati hilo linapogawanywa ki jinsia, ni miaka 74 na miezi miwili kwa wanawake na miaka 69 na miezi minane kwa wanaume.

Basi kwanini kwa wastani wanawake wanaishi maisha marefu zaidi kuliko wanaume, na kitu gani kinawapa faida hii?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanawake zaidi kuliko wanaume wana nafasi ya kusherehekea miaka 100 tangu kuzaliwa.

Hebu tuangalie sababu tatu kuu.

1. Jeni

Faharasha ya uhai wa binaadamu kwa sasa inajumuisha taarifa kuhusu mataifa 40, ikiwemo data kutoka Sweden na Ufaransa tangu mwaka 1751 na 1816.

Lakini data za nchi kama Japan na Urusi inapatikana kuanzia kati kati ya karne ya 20 pekee.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanawanake wana jozi mbili za X chembeuzi

Hatahivyo, kwa kila nchi kwa kila mwaka katika data hiyo, wakati wa kuzaliwa, urefu wa maisha kwa wanawake unaongezeka ikilinganishwa na wanaume.

Inavyoonekana, tangu mwanzo, wanaume ndio wanaoathirika zaidi kutokana na muundo wao wa jeni mwilini.

Mayai ya uzazi

"Mayai ya kiume huharibika kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ya kike," anasema Profesar David Gems wa University College London.

Mojawapo ya sababu ni kutokana na jukumu la chembeuzi au kromosomu, - nyuzi zinazobeba DNA ambazo hubaini jinsia ya mtoto.

Wanawake wana kromosomu XX na wanaume XY.

Na kromosomu huwa zina jeni.

Kromosomu X zina jeni nyingi zinazokusaidia kuishi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege wa kiume wana aina mbili ya kromosomu X

Katika ndege, wa kiume wana aina mbili ya kromosomu X na wanaishi maisha marefu zaidi kuliko wanawake.

2. Homoni

Haki miliki ya picha ISSOUF SANOGO

Katika miaka ya ujana, wavulana na wasichana wanakuwa wanaume na wanawake kutokana na mabadiliko ya homoni mwilini.

Testosterone, ambayo hufanya mwili kuwa mkubwa na wenye nguvu ndio huchangia tabia nyingi za kiume - mfano sauti kuwa nzito na nywele kuota kifuani.

Uhai unaongezeka kwa wanaume wakati wa kuongezeka kwa testosterone mwilini, ambayo hujitokeza katika miaka ya baadaye kwa vijana.

Wataalamu wanasema hii huenda inatokana na wanaume kujihusisha na shughuli nzito na hatari kama kupigana, kuendesha baiskeli na magari kwa kasi kubwa, pamoja na kujitoa uhai.

Na katika majaribio kwa wanyama wanawake, waliokosa oestrogen huonekana kutoishi maisha marefu.

Haki miliki ya picha Getty Images

3. Ajira na tabia

Katika maeneo yalioathirika na mizozo, kiwango cha maisha kwa wanaume kinashuka.

Lakini katika maeneo ambako kuna huduma ndogo ya afya, wanawake wengi wanafariki wakati wa kujifungua.

Mambo kama uvutaji sigara, kula kupita kiasi huenda kwa kiwango fulani ikaeleza kwanini kiwango cha pengo kijinsia kinatofautiana kwa ukubwa baina ya mataifa.

Maisha marefu lakini yasiokuwa ya afya bora

Lakini sio faida tu ya upande mmoja. Licha ya kwamba wanawake wanaishi maisha marefu, wanataabika zaidi kwa ugonjwa, zaidi kadri miaka inavyosogea.

Haki miliki ya picha CHARLES BOUESSEL

Wanawake walio na umri wa kati ya miaka 16 hadi 60 huenda wakamuona daktari zaidi ikilinganishwa na wanaume wa umri sawa katika nchi tofauti.

Steven N. Austad na Kathleen E. Fischer kutoka chuo kikuu cha Alabama wamesema katika waraka uliochapishwa kwenye jarida la Cell Press kwamba " katika mataifa ya magharibi, wanawake huwaona madaktari zaidi , wanakosa kwenda kazini kutokana na kuwa mgonjwa na hunywa dawa zaidi kuliko wanaume".

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii