BBC inazindua tuzo ya Komla Dumor 2019
Huwezi kusikiliza tena

Je wewe ni Mwanahabari tunayekutafuta?

BBC inamtafuta nyota chipukizi wa uandishi habari Afrika kwa tuzo ya BBC World News Komla Dumor Award, sasa katika mwaka wa tano.Waandishi habari kutoka maeneo tofuati barani Afrika wanakaribishwa kuwasilisha ombi katika tuzo hiyo, inayonuia kufichua na kuendeleza vipaji vipya kutoka Afrika.

Mshindi atahudumu kwa miezi mitatu katika makao makuu ya BBC mjini London ambako atapata mafunzo na uzoefu wa kazi.Mwisho wa kuwasilisha maombi in Februari 26 2019, saa 23:59 GMT.

Tuzo hiyo iliidhinishwa kumuenzi Komla Dumor, mwandishi habari wa aina yake raia wa Ghana na mtangazaji wa BBC World News, aliyefariki ghafla akiwa na umri wa miaka 41 mnamo 2014.

Tuzo ya mwaka huu inazinduliwa kutoka mji mkuu wa Nigeria, Lagos.

Mada zinazohusiana