Papa Francis akiri kupokea barua kutoka kwa rais Maduro wa Venezuela

Venezuela politics Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Papa Francis aahidi kushughulikia mzozo wa nchini Venezuela endapo pande zote mbili zitaridhia

Papa Francis amesema kuwa yuko tayari kuwa mpatanishi katika mazungumzo kati ya Rais Nicolas Maduro na kiongozi wa upinzani, Juan Guaido, ikitokea pande zote mbili kuomba kupatanishwa.

Aliyasema hayo kwa waandishi wa habari wakati akiwa njiani kurejea kwenye makaazi yake akirejea katika safari yake ya kihistoria huko Abu Dhabi.

Hata hivyo ,Papa alisema kwamba Vatican na wanachama wengine wa jumuiya ya kimataifa wangehitaji kuchukua hatua za awali kabla ya kuanza mchakato wa majadiliano.

  1. Kwanini ziara ya Papa huko Arabuni ni muhimu ?
  2. Papa Francis alaani vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto
  3. Kwanini ziara ya Papa huko Arabuni ni muhimu ?

Papa Francis alitanabahisha pia kuwa ameipokea barua kutoka kwa Maduro lakini alisema hajaisoma:

'Kabla ya ziara yangu, nilitambua kuwa rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametuma barua na alikuwa ametuma barua katika kikapu cha kidiplomasia'.

'Nakiri bado sijaisoma barua hiyo, tutaona nini cha kufanya, ni muhimu sana' alisema.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kwa hali ilivyo inapaswa pande zote mbili ziombe upatanishi wa kimataifa kama ilivyo wahi kutokea kwa nchi za Argentina na Chile.

Papa anachokiona nchini Venezujela kilikuwa sehemu ya majadiliano, yaliyofanyika kati ya Zapatero na Monsinyori Sheri na baadaye kuendelezwa na askofu Celli.

Kutoka huko alizaliwa kiumbe mdogo, hakuna moshi.

Sasa, sijui: nitaifungua barua hiyo baada ya hapo nitaangalia cha kufanya, lakini hali ya awali inahitaji kuwa pande zote mbili zitake suluhu.

Na sisi tuko tayari kwa ombi lao .

Nchi ya Venezuela raia walio wengi ni wa madhehebu ya dini ya kikatoliki, wanaogopa kwamba msimamo kati ya bwana Maduro na kiongozi wa mpito Guaido unaweza kushuka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Guaido, ambaye anaungwa mkono na serikali ya Marekani na washirika wake, alijitangaza kuwa rais wa kipindi cha mpito wiki mbili zilizopita, akimshtaki raisi aliyekuwa madarakani Nicolas Maduro kwa ukiukaji wa taratibu za uchaguzi wa mwaka jana.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii