Waandishi wa BBC waachiwa kwa dhamana Uganda

BBC New Broadcasting House Building Haki miliki ya picha Getty Images

Waandishi wa BBC waliotiwa mbaroni na polisi nchini Uganda wameachiwa kwa dhamana.

Waandishi hao walikuwa wakifuatilia taarifa kuhusu uuzaji haramu wa dawa za serikali na walikamatwa Jumatano usiku.

Polisi Uganda ilikuwa imewazuia waandishi hao katika mji mkuu, Kampala.

Msemaji wa serikali ya Uganda alikaripia vikali kitendo hicho cha polisi akisema habari hiyo ina maslai kwa taifa.

" Bado sijafahamu ni kwa misingi gani polisi iliwakamata waandishi habari hawa, ambao kwa mtazamo wangu walikuwa wanaisaidia serikali kufichua muozo ulioko kwenye mfumo," msemaji wa serikali Ofwono Opondo ameliambia Reuters. "Wanapaswa kuachiliwa pasi masharti."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii