Bomu lawalipukia na kuwaua bwana harusi na mpambe wake nchini Ethiopia

Grenades recovered in Somalia (file photo) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bunduki na mabomu hupatikana kiholela katika pembe ya bara Afrika kutokana na miongo kadhaa ya vita.

Bwana harusi na mpambe wake wamefariki dunia nchini Ethiopia kwenye mlipuko wa bomu la kutupa kwa mkono.

Mamlaka nchini humo zinaarifu kuwa bomu hilo lilikuwa linamilikiwa na bwana harusi.

Mlipuko huo ulitokea kwenye karamu iliyoandaliwa na mpambe baada ya kumalizika katika sherehe za fungate ya siku 10.

Bibi harusi hakuwepo eneo la tukio wakati bomu hilo likilipuka na hivyo amepona.

Tukio hilo limetokea kwenye Kijiji cha mbali katika mkoa wa Amhara, kaskazini ya mji mkuu Addis Ababa.

Bomu hilo lilikuwa likimilikiwa kinyume cha sharia na bwana harusi huyo, polisi wameileza BBC.

Bwana harusi huyo amefahamika kama Mohammed Hassan Mohammed mwenye umri wa miaka 25. Na mpambe wake amefahamika kama Bogale Sebsibe Abera, 24.

Mamlaka nchini Ethiopia zimekuwa zikishutumiwa vikali kwa kushindwa kudhibiti wa umiliki wa silaha kinyume cha sheria. Wengi wa wamiliki hao wasio halali hufyatua risasi angani katika matukio makubwa kama misiba na harusi. Bwana harusi na mpambe wake walipuliwa na bomu

Mada zinazohusiana