Ubakaji Sierra Leone: Zaidi ya visa 8,500 vya ubakaji viliripotiwa mwaka uliyopita

Ubakaji Sierra Leone Haki miliki ya picha Reuters

Sierra Leone imetangaza ubakaji na dhulma zingine za kijinsia kuwa janga la kitaifa baada ya viwango vya visa hivyo kuvunja rekodi mwaka jana.

Zaidi ya visa 8,500 vya ubakaji viliripotiwa mwaka jana- ikililinganishwa na karibu visa 4,000 vilivyo rekodiwa mwaka uliyotangulia katika taifa hilo lililo na watu milioni 7.5.

Wanaharakati hata hivyo wanasema makosa mengi hayachukuliwi hatua chini ya sheria ya sasa.

Rais Bio ametoa tangazo hilo baada ya mwanamke aliyenusurika ugonjwa wa hatari wa ebola kubakwa mara kadhaa.

Bw. Bio pia amesema visa vya watoto wadogo kunajisiwa vimemefikia thuluthi tatu na kuongeza kuwa wale watakaopatikana na hatia watafungwa maisha jela.

Sababu za kuongezeka kwa uhalifu huo hazijabainika.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio

"Kuanzia sasa ukipatikana na hatia ya kumnajisi mtoto utafungwa maisha gerezani," alisema.

Rais pia ametangaza hatua ya kubuniw akwa kitengo maalum cha polisi kitakachopewa jukumu la kuchunguza visa vya uhalifu wa kingono.

Pia ameomba idara ya mahakama kubuni mahakama maalum zitakazoshughulikia kesi hizo na kutoa uamuzi wa haraka.

Mwandishi wa BBC Umaru Fofana mjini Freetown amesema tangazo hilo linamaanisha raslimali ya taifa itatumika kupambana na unyanyasaji wa kingono.

Pia anasema hatua hiyo pia inamaanisha bunge halitashirikishwa katika mpango huo licha ya kuwa jukumu la kutunga na kufanyia marekebisho sheria.

Watu wamepokeleaje hatua hiyo?

Hasira zimekuwa zikiongezeka kuhusiana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake baada ya visa hivyo kuongezeka mara dufu, hasa baada ya mtoto wa miaka mitano kulemaa baada ya kudaiwa kunajisiwa na mjomba wake.

Wanaharakati wa kutetea haki wanasema ni visa vichache vinavyo chukuliwa hatua kisheria.

Haki miliki ya picha AFP

Adhabu ya ubakaji ni kifungo cha miaka 15 jela na mara nyingi hukumu hiyo haizingatiwi.

Mwaka uliyopita mwanamume wa miaka 56 aliyepatikana na hatia ya kubaka mto wa miaka sita alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.

Fatmata Sorie, rais wa chama cha mawakili wanao wawakilisha waathiriwa wa ubakaji mahakamani, ameiambia BBC kuwa tangazo la rais litapiga jeki juhudi za kukabiliana na uhalifu huo

Hata hivyo ametoa tahadhari kuwa data za dhulma za kijisia haijakamilika kwa sababu imekusanywa kutoka kwa vituo vichache kote nchini.

"Tunataka kupunguza idadi ya visa hivyo lakini tunapendekeza data ya hali halisi ya mambo ikusanywe kutoka kila pembe ya nchi," alisema.

Visa vya ubakaji na unyanyasaji wa kijishuhudiwa sana Sierra Leone kati ya mwaka 1991 na 2002 wakati nchi hiyo ilipotumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii