Wanasayansi wamevumbua dawa mpya ya kukabiliana na malaria

Mbu wa kike pekee ndio wanaouma watu na wanavutiwa sana na damu ya binadamu kwa sababu ina madini ya protini wanayohitaji ili kuzaana Haki miliki ya picha Alexander L Wild
Image caption Mbu wa kike pekee ndio wanaouma watu na wanavutiwa sana na damu ya binadamu kwa sababu ina madini ya protini wanayohitaji ili kuzaana

Wanasayansi wamevumbua njia ya kumdhibiti mbu anayesababisha malaria kwa kutumia dawa iliyo na chembe chembe ya damu ya binadamu.

Dawa hiyo inaaminiwa kuwashibisha mbu na kuwafanya kukosa hamu ya kumuuma mtu, wamesema wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Rockefeller nchini Marekani.

Mfumo huo wa tiba utakapo idhinishwa unaweza kutumika kuzuia homa ya zika, homa ya manjano na malaria.

Utafiti huo japo bado uko katika awamu ya kwanza uanatoa matumaini ya kupatikana kwa tiba ya magonjwa hayo hasa katika maeneo yanayowaathiri watu kwa wingi.

Mbu wa kike pekee ndio wanaouma watu na wanavutiwa sana na damu ya binadamu kwa sababu ina madini ya protini wanayohitaji ili kuzaana.

Watakapomuuma mtu aliyemeza dawa hiyo mpya inayofanyiwa uchunguzi watashindwa kufanya kazi kwa siku kadhaa.

Hawana hamu ya kula

Watafiti walipowapatia mbu mchanganyiko wa maji yaliyo na dawa hiyo walishangazwa kuona kuwa mbu hao walishindwa kula baada ya kutumia maji hayo.

Ili kubaini ikiwa mfumo huo wa tiba unaweza kufanya kazi, walitundika mfuko iliyokuwa na harufu ya mwili wa binadamu karibu na mmoja wao ilikuchunguza ni nini kinachowafanya kupoteza hamu ya kula.

Uvumbuzi huu utawasaidia wanasayansi kubaini kilipo kiungo hicho kwenye mwili wa mbu ili wabuni njia ya kukifanyisha kazi na kudhibiti shughuli zake.

'Twaishiwa na maarifa'

Watafiti wanasema matokeo yao yatakuwa na athari kwa tafiti zijazo.

"Tumeanza kuishiwa na maarifa ya jinsi ya kukabiliana na wadudu wanaosambaza magonjwa, na hii ndio njia mpya kabisa ya kuwadhibiti,"anasema mmoja wa watafiti hao, Leslie Vosshall, kutoka chuo kikuu cha Rockefeller.

"Dawa ya wadudu zimeshindwa kufanya kazi kwasababu mbu wamezizoea, na sisi bado hatujapata chanjo ambayo inakinga magongwa yanayosambazwa na mbu."

Bi Duvall amesema wazo la kujikita katika lishe ya ambu itazaa matunda kwasababu wanahitaji kula ili kuishi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii