Sanganer: Jela ambayo wafungwa hutoka nje ili kutafuta ajira India

Jela ya Sanganer

Katika jela ya Sanganer , katika mji wa Jaipur nchini India ,wafungwa wanapewa mahali pa kulala lakini hawapewi chakula na fedha.

Hii inamaanisha kwamba ni lazima waende kufanya kazi ili kujipatia kipato nje ya jela hiyo kulingana na Masuma Ahuja. Baadhi ya kazi wanazopata afumngwa hao ni kama vile vibarua, kazi za viwanda , madereva na hata walimu wa Yoga.

Ramchand hupeleka basi la shule. Mkewe Sugna anafanya kazi katika kiwanda cha nguo.

''Mimi hunywa chai nao katika chumba kimoja wanachoishi ambacho kina kuta za rangi ya manjano huku kikiwa na paa lililozibwa na simiti, jokovu na runinga''.

Hivi ndivyo wanavyotoa hadithi yao. Alikuwa pekee, kwani familia yake ilikuwa imemuacha.

''Majirani zao walikuwa wanataka kuwaoza ili awe mwanamke asiyeishi pekee, ili awe na mtu atakayemwangalia , kumpikia na kumtengenezea roti''., anasema alimuoa kwa sababu alimpenda.

Hakuna geni kuhusu nyumba yao ama hata hadithi yao. Isipokuwa tu kwamba Ramchand na Sugna ni wafungwa waliopatikana na hatia ya uhalifu wa mauaji na sasa wanaishi jela.

Nyumba yao ipo katika jela ya Sanganer Open Prison mjini Jaipur, ambao ndio mji mkuu wa jimbo la magharibi mwa India la Rajasthan.

Jela hii haina maeneo ya kuwazuia kutotoka nje ama hata nyuta, haina walinzi katika lango lake kuu na wafungwa huruhusiwa na hata kushawishiwa kwenda mjini na kutafuta kazi .

Jela hiyo ambayo imekuwa wazi tangu mwaka 1950 ni nyumbani ya wafungwa 450 na ni miongoni mwa jela 30 kama hizo katika jimbo la Rajasthan.

''Naenda Sanganer na Smita Chakraburtty, mwanamke anayeoongoza kampeni za kuzifanya jela zionekane kuwa mahali kwa kawaida''.

Amewasilisha ombi lake katika mahakama ya kilele ya India ambayo badala yake imeyataka majimbo kufungua taasisi zaidi kama hizi .

Kwa sasa anahudumu kama kamishna wa magereza katika jimbo la Rajasthan na hivi majuzi aliorodheshwa katika tuzo ya Agami kwa kazi yake nzuri ya mfumo wa jela nchini humo.

''Mfumo wa jela nchini humo unaangazia kuhusu kisa....na haujui cha kumfanyia mtu'', Chakrabutty anasema.

Kampeni yake inaendelea kuwa maarufu .Majimbo mengine manne nchini India yalifungua jela huru mwaka uliopita.

''Ninapotembelea Sanganer na Smita yeye huwapatia wafungwa yanayoendelea na kazi zao nao huja kwangu wakitaka kuzungumza nami''.

''Huku ikiwa hakuna walinzi mtu yeyote anaweza kuingia katika jela hiyo , na wageni kama mimi ni wachache mno''.

Nimekaa katika sakafu katika shule ya chekechea mbele ya jela hiyo na ninazungumza na kundi moja la wafungwa wanaume na wanawake.

Ninapowauliza kwa nini wako jela wanajibu 302 wakielezea kuhusu kifungu cha 302 katika sheria za India ambacho kinasema wahalifu wa mauaji lazima waadhibiwe.

Wanaita jela hizo mashamba huru na kudai vile ilivyorahisi kuishi hapo na vile wanavyofurahia.

Ili kufika Sanganer , ni sharti wawe wamehudumia thuluthi mbili za miaka yao katika jela za kawaida na wanasema kwamba wakilinganisha na jela hizo nyengine wanasema kuwa wapo huru.

Serikali ya Rajasthan mara nyengine imelazimika kuwafurusha wafungwa ambao wanakataa kuondoka.

Wamepata kazi, wamepata shule za watoto wao. Lakini bado wafungwa wengi wananielezea kwamba bado wanapata changomoto kuhusu vile watu walio huru wanavyochukulia jela.

Baadhi ya wanawake wafungwa wanasema kuwa ni rahisi kufunga ndoa na wafungwa wenzao kwa kuwa wanaume walio nje ya jela hiyo hawawaelewi vizuri.

Mara nyengine hata kupata kazi inaweza kuwa vigumu, wanasema kuwa watu wanaogopa kuwaajiri wanapotoa vitambulisho vyao.

Lakini bado wanaendelea kuishi maisha ya kawaida .

Wananunua pikipiki, simu aina ya smartphone, runinga, na hawavai magwanda ya jela na idadi ya watu wanaoishi katika nyumba walizopewa ni chache.

Kila mfungwa hupewa nyumba na serikali katika jela hiyo. Jela hiyo haiwapatii chakula maji ama kipato. Hivyobasi kila siku wengi wao huondoka katika jela hizo ili kutafuta kipato .

Image caption Wafungwa sharti wahudhurie wito wa jioni wa kujua iwapo wapo

Wanaume waliopatikana na hatia ya muaji hufanya kazi kama walinzi , wafanyikazi wa viwandani ama vibarua.

Ninakutana na mfungwa mmoja ambaye ni mwalimu wa kufunza yoga na mwengine ambaye ni msimamizi karibu na shule moja.

Sheria iliopo ni kwamba wafungwa lazima wahesabiwe kila jioni. Sanganer haifanani na jela , isipokuwa wakati huu .

Wakati jua linaposhuka , wawakilishi wa serikali katika jela hiyo husimama mlangoni. mfungwa mmoja aliye na kipaza sauti huanza kuita nambari zao moja hadi 450.

Mara nyengine husita na kumshutumu mfungwa aliyewacha uchafu nje ya nyumba yake.

''Kila mtu awajibike ama arudishwe katika jela ya kawaida''.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii