Haile Selassie: Kwa nini AU imejenga sanamu yake?

Mfalme Haile Selassie I, Mfalme wa Ethiopia
Image caption Haile Selassie alikuwa mfamle wa mwisho wa Ethiopia

Sanamu ya mfalme wa mwisho wa Ethiopia imejengwa nje ya makao makuu ya muungano wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia.

Lengo la sanamu hiyo kujengwa nje ya makao hayo ni kutambua mchango wake katika uanzishaji wa OAU ambalo ndio mtangulizi wa Muungao huo wa Afrika.

Lakini huenda hilo sio jambo la kwanza linalojitokeza katika fikra unaposikia jina Haile Sellasie. Jina hilo linahusishwa sana na mwanamuziki wa Jamaica Bob Marley na Rastafarians.

Hivyobasi ni nani haswa Haile Selassie na ni vipi alianza kuabudiwa kama mungu na watu wanaoishi mbali?.

Kwa nini amejengewa sanamu?

Haile Selassie alikuwa katika uongozi wake kwa takriban miaka 30 wakati aliposaidia kuanzisha OAU.

Mkutano wake wa kwanza mnamo mwezi Mei 1963 ulifanyika mjini Addis Ababa.

Ethioipia ambayo haijatawaliwa licha ya kuongozwa kijeshi na Itali kwa miaka mitano imeonekana kuwa ishara ya Uhuru wa Afrika tangu kipindi cha ukoloni.

Image caption Sanamu ya Haille Salassie yazinduliwa katika makao makuu ya umoja wa Afrika mjini Addis Ababa

Mataifa mengine yalikuwa yakipata uhuru wao na ikawa fursa ya kuyaunganisha pamoja ili kukabiliana na ukoloni na uongozi wa weupe walio wachache mbali na kushirikisha juhudi za kuinua hali ya maisha na kutetea uhuru wao.

''Ningependa mkutano huu wa Muungano kuwepo kwa miaka 1000'', Selassie, ambaye alitumia mwaka mmoja akiandaa mji huo kwa mkutano huo aliambia wajumbe.

Kama ilivyokuwa OAU ilibadilika na kuwa AU mwaka 2002.

Lakini mchango wake katika kuanzisha muungano huo haujasahaulika , na sanamu hiyo ni njia moja ya AU kutambua mchango wa Selassie.

Je ni vipi alionekana kuwa 'mungu'?

Yote yalianza mwaka 1930 wakati mwanaharakati mweusi wa Jamaica Marcus Garvey alipowatabiria wafuasi wake kwamba mfalme mweusi atatoka Afrika na kwamba siku ya ukombozi itakuwa imewadia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rastafarians wanaamini kwamba Haile Selassie ni masihi

Hivyobasi mtu mweusi kwa jina Ras Tafari alipokuwa mfalme Ethiopia, wengi waliona kwamba utabiri huo umekuwa wa kweli.

Katika mataifa ya Afrika mashariki Ras Tafari au Chifu Tafari alikuwa Haile Selassie{ Mungu wa utatu}. Umbali wa maili 8000 huko West Indies, Haile Selassie alifanywa Mungu (au Jah) masihi mkombozi na Ethiopia kama taifa lililoahidiwa.

Kwa ufupi , vuguvugu la Rastafarian lilizaliwa. Je Selassi aliliamiani? hakujaribu kupinga imani hiyo alipotembelea Jamaica 1966.

Mfamle huyo alisalimiwa na maelfu wakitaka kumuona mungu wao.

Miongoni mwa wale waliojitokeza ni mke wa mwanamuziki wa muziki wa Reggae Bob Marley ambaye alikuwa ameelekea Marekani.

Rita Marley baadaye alisema vile alivyoona alama za kucha za kikofi cha Sellasie alipokuwa akimpungia mkono.

Ulikuwa wakati wa muamko wa kidini na mumewe aliporudi walikubali imani hiyo.

Miaka mitatu awali Rastafarians walikuwa wameanza kuelekea nchini Ethiopia na Selassie alikua ametenga kipande cha ardhi ambacho watu weusi kutoka magharibi wangeishi 1948.

Baada ya ziara hiyo , idadi hiyo ilizidi kuongezeka. Hii leo jamii hiyo ina takriban watu 300.

Lakini wafuasi wake walikanganyika baada ya Selassie kufariki mwaka 1975 , mwaka mmoja baada ya kupinduliwa .

Yote yasemwe lakini Mungu hawezi kuaga dunia. Hili lilitatuliwa baada ya kukubaliana kwamba mwili wa Selassie ulikuwa mwili wake wa kidunia.

Pia ijulikane kwamba Garvey hakua muumini. Ukweli ni kwamba alikuwa mkosoaji mkubwa wa Selassie.

Je alikuwa mtu wa aina gani?

Mjadala umegawanyika kuhusu iwapo Selassie aliisaidia Ethiopia au la.

Ripoti moja ya shirika la Human Rights Watch inamtuhumu kwa kuangazia kwa utofauti mkubwa janga la ukame katika maeneo kadhaa ya taifa hilo na kujaribu kuficha ukame wa 1972-72 ambapo takriban watu 200,000 walidaiwa kufariki.

Pia anajulikana kwa kuwakabili watu waliompinga wakati wa utawala wake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sanamu ya Selassie itajiunga na ile ya rais wa Ghana Kwame Nkrumah, mwanzilishi mwengine wa AU

Marcus Garvey hakupendelea wakati alipotoroka Ethiopia 1936 kufuatia uvamizi wa majeshi ya Benito Mussolini mwaka mmoja mapema akimtaja Selassie kuwa mtu mwoga na gaidi wa utumwa .

Kitendo hicho hakikuharamishwa nchini Ethiopia hadi mwaka 1942.

Msomi Dkt Yohannes Woldemariam amehoji kwamba Sellasie anafaa kukumbukwa kama dikteta .

Alitengeneza katiba ambayo ilimpatia madaraka yote na vizazi vyake. Lakini wafuasi wake wanadai kwamba alikuwa kiongozi mzuri wa Kiafrika aliyekuwa maarufu duniani.

Wito wake kwa mataifa makuu baada ya taifa lake kuvamiwa unakumbukwa hadi leo-mbali na kwamba ni mojawapo ya nyimbo za Bob Marley za mwaka 1976 War.

Cha mno ni kwamba hakuwa mfalme kutokana na kizazi chake.

Licha ya kuzaliwa katika familia ya kawaida 1892, alitajwa kuwa kiongozi baada ya kumfurahisha mfame Menelik 111 na intelijensia yake.

Na sanamu yake itawakumbusha watu kwamba alikuwa kiongozi aliyepigania ushirikiano na kuwacha urithi ambao unaendelea kuwaathiri mamilioni ya Waafrika leo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii