Wazazi wanapolazimika kuwashtaki watoto zao ili wawatunze

Mchoro wa mtu mzima na mkewe wakishika fedha pamoja na mwanao

Abu Taher anasema kuwa mwanawe alikuwa 'mtoto mzuri'.

Kwa miaka mingi bwana Taher alikuwa akifanya biashara ya kuuza nguo katika duka moja dogo katika mji wa Chittagong, nchini Bangladesh.

Alistaafu na fedha kidogo na kuanza kumtegemea mwanawe wa kiume na yule wa kike ili kujikimu.

'Mimi na mkewe wangu tulipitia hali ngumu kumlea mwanangu wa kiume', alisema bwana Taher.

Lakini baada ya kufunga ndoa alibadilika na kuwacha kutuangalia sisi wazazi wake. Licha ya kupata usaidizi kutoka kwa mwana wao wa kike, bwana Taher alipata shida.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 75 anasema kuwa alikuwa hana chagua jingine bali kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwanawe Mohammad Shahnjaan ili kujikimu.

''Ulikuwa uamuzi mgumu kwangu. Kila mtu alikuwa akiniambia kuwasilisha kesi mahakamani , lakini sikutaka. Nilianzisha kehi nilipoona sina chaguo''.

Mwanawe anakana madai hayo.

Wawili hao wamekuwa na uhusiano mbaya kwa miongo kadhaa lakini bwana Shahnjan ambaye anafanya kazi kwenye benki anasema kuwa amekuwa akiwasaidia wazazi wake.

Anasema kuwa babake alianzisha kesi hiyo ''kumuaibisha''.

Mzazi dhidi ya Mtoto

Ni mgogoro wa kifamilia ambao unaweza kufanyika mahali popote lakini hatua iliochukuliwa na bwana Taher ni ya kipekee

Aliwasilisha kesi chini ya kifungu cha sheria ya kuwaangalia wazazi nchini Bangladesh , sheria inayowasaidia wazazi ambao wametelekezwa na wanawao.

Majimbo mengi ya Marekani na Ulaya pia wamekuwa na sheria kama hizo lakini yameshindwa kuidhinisha. Lakini barani Asia mara nyengine hutumika.

Mtafiti wa kiafya katika chuo kikuu cha Emory Dkt. Ray Serrano amechanganua sheria kadhaa ambazo zinawataka watoto kuwasaidia wazazi wao ama kuheshimu watu wazima.

Anataja sheria kama upanuzi wa watoto kuwasaidia wazazi katika jamii ambazo zinaona umuhimu wa familia na jamii.

Jukumu la kutoa usaidizi

Singapore ni mojwapo ya mfano.

Wazazi wenye umri mkubwa ambao hawawezi kujisaidia wanaweza kutafuta usaidizi wa kifedha kutoka kwa sheria ya taifa hilo ya kuwasaidia wazazi.

Wanaweza kuwasilisha madai katika visa ambavyo watoto wanaweza kuwaangalia, lakini wanakataa.

Image caption Maombi ya kupata usaidizi yaliowasilishwa nchini singapore katika jopo la kusikiza kesi za kuwasaidia wazazi

Jopo linaweza kutoa uamuzi wa wazazi kupewa marupuru ya kila mwezi ama kitita kikubwa.

Fedha hizo za kuwasaidia wazazi pia zinaweza kuafikiwa kupitia maelewano.

Visa vichache hupitia majopo kwa kuwa vingi hutatuliwa kupitia maelewano.

Mwaka 2017 ni kesi 20 pekee zilizowasilishwa katika jopo hilo na kupata majibu ya usaidizi.

Utamaduni

China, India na Bangladesh zina mfumo kama huo ambao umeimarika katika miaka ya hivi karibuni katika harakati za kuafikia mahitaji ya jamii inayozeeka . Dr Serrano anasema ni wazo la usawa.

Iwapo umekuwa mtoto mwenye utu uzima na huishi na wazazi wako ni vyema kuwasaidia.

Watoto hukabiliwa na faini na hata kufungwa jela katika hali nyengine.

Kwa mfano katika mkoa wa Sichuan nchini China, watu watano walifungwa miaka miwili jela kwa kumuwacha baba yao mzee , baada ya mahakama kugundua kwamba hawakuwa wakitekeleza wajibu wao.

Jukumu la serikali

Sheria hiyo inaangazia ufukara miongoni mwa wazee na sio suluhu ya muda mrefu.

Lakini huku jamii ikiendelea kuzeeka wanaweza kutumia kifaa kitakachoishinikiza serikali.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa 2020, idadi ya watu walio na umri wa miaka 60 na walio wazee itaipiku ile ya watoto walio na chini ya umri wa miaka mitano.

Na mwaka 2020, asilimia 80 ya wazee wataishi katika mataifa yalio na mapato ya kadri.

Dkt. Serrano anasema kuwa mifumo kama hiyo nchini Singapore inaweza kuwa kama kiboko kinachowashinikiza watu kuwasaidia wazazi wao wanaozeeka.

Pia yanaweza kuwa mabadiliko ya sera ambayo yanaweza kupingwa katika mataifa kama vile Marekani na Uingereza.

Msomi wa chuo kikuu cha Havard James Sabin anasema kuwa sio rahisi kwamba sheria kama hizi zinaweza kuungwa mkono Marekani.

Lakini kwa bwana Taher , mfumo huo wa Bangladesh ulimsaidia sana.

Aliafikia makubaliano ya nje ya mahakama na mwanawe bwana Shahnjan kumpatia ($119; £92) kila mwezi .

Kufikia sasa ameheshimu mpango huo na bwana Taher anasema kuwa iwapo mwanawe ataendelea kumapatia fedha hizo ataiondoa kesi hiyo katika mahakama ya Chittagong.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii