'Michoro ya Hitler' yakosa mnunuzi mnadani Ujerumani

Mnada huo umekumbwa na tuhuma kwamba unauza viu bandia. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mnada huo umekumbwa na tuhuma kwamba unauza viu bandia.

Picha tano zinazodaiwa kuchorwa na kiongozi wa Nazi Adolf Hitler zimekosa mnunuzi katika mnada nchini Ujerumani.

Mnada wa Jumba la Wiedler ulilenga kuchangisha £40,000 kutoka kwa mchoro huo unaouzwa bei ghali.

Madai ya kughushi bidhaa hizo yalikumba mnada huo na meya wa mji huo Ulrich Malu alitaja kuwa yenye nia mbaya.

Mauzo hayo yalifanyika mjini Nuremberg , Ujerumani , mji ambao una sifa za kuandaa mikutano ya Nazi ambapo viongozi wakuu wa Nazi walishtakiwa kwa uhalifu wa vita.

Mauzo hayo pia yalishirikisha bidhaa zinazodaiwa kumilikiwa na dikteta huyo ikiwemo chombo cha kuwekea maua kiti kilicho na alama ya Nazi katika mkono wake.

Chini ya uongozi wa Hitler kati ya 1933-45, Nazi walianza vita vya dunia vya pili wakiwa na nia ya kutekeleza sera yao ya mauaji ya kimbari ambayo yalisababisha mauaji ya Wayahudi milioni sita pamoja na makumi ya mamilioni ya raia wengine na wapiganaji.

Onyesho la alama hiyo ya Nazi hadharani haliruhusiwi Ujerumani isipokuwa kwa maswala ya elimu ama sababu za kihistoria.

Jumba la mnada huo lilifanikiwa kuzunguka sheria kwa kuficha alama hiyo.

Je mnada huo ulikabiliwa na changamoto gani?

Makumi ya michoro , ikiwemo ile ilioandaliwa kuuzwa ilikamatwa kutoka kwa jumba hilo la mnada wiki iliopita na maafisa wa polisi wa Ujerumani.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa takriban michoro 63 ilio na saini ya AH ilikamatwa kutokana na madai ya kughushi.

Uchunguzi ulianzishwa dhidi ya watu ambao hawakutambulika kwa tuhuma za kughushi bidhaa hizo mbali na kufanya udanganyifu, muendesha mashtaka wa Nuremberg aliambia AFP.

Alithibitisha kuwa jumba la mnada huo lilishirikiana nao kutoa michoro kwa kujitolea.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Michoro mitano iliosalia katika mnada haikuvutia wanunuzi

Mauzo ya michoro hiyo inayodaiwa kutoka kwa dikteta huyo mara kwa mara huzua hisia na tuhuma za kughushi.

Mwezi uliopita maafisa wa polisi wa Ujerumani walipata vitu vya Hitler wakiwa na wasiwasi kuhusu kule ambako vilikuwa vikitoka.

Hitler ambaye alikataliwa mara mbili na shule ya uchoraji ya Vienna anajulikana kuuza kazi yake akiwa kijana.

Kazi zake nyingi zilizodaiwa na wataalam kuwa za kiwango cha chini zimeuzwa katika miaka ya hivi karibuni.

Mwaka 2015, Jumba la mnada la Wiedler liliuza zaidi ya makumi ya michoro inayodaiwa kutoka kwa Hitler kwa €400,000.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiti kilicho na alama ya nazi katika mikono yake.

Wanunuzi walitoka kutoka Ujerumani, China, Ufaransa, Brazil na UAE.

Mwaka 2014 jumba hilo la mnada liliuza mchoro wa rangi za maji kuhusu mji mkuu wa Munich kwa €130,000.

Uuzaji wa kumbukumbu za Nazi ni swala linalosalia kuzua mgawanyiko duniani.

Wanunuzi wengine wanasema kuwa wananunua kutokana na sababu za koihistoria , lakini wanaharakati wanaonya kwamba vitu hivyo pia hununuliwa na watu wa mrehgo wa kulia ambao wanatii utawala wa Hitler.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii