Uchaguzi Nigeria 2019: Tunazimulika changamoto kubwa za taifa hilo kwa ramani

Ramani za BBC zinaonyesha changamoto kuu kwa Nigeria, taifa lenye idadi kubwa ya watu na uchumi mkubwa barani Afrika, wakati taifa hilo likikaribia uchaguzi mkuu miaka 20 baada ya kumalizika kwa utawala wa kijeshi na kurudi kwa demokrasia.

Miaka minne iliyopita, chama cha Rais Muhammadu Buhari, All Progressives Congress (APC) kilipokithiri katika maeneo ya kaskazini na kusini magharibi mwa nchi hiyo ambapo mpinzani mkuu wa chama hicho, chama cha People's Democratic Party (PDP), kilikuwa na umaarufu mkubwa kusini na kusini mashariki.

Hatahivyo, tofauti na uchaguzi wa mnamo 2015 wakati kiongozi wa kutoka eneo la kaskazini, Buhari, alikabiliana na mgombea kutoka eneo la kusini, rais aliyeondoka Goodluck Jonathan, mara hii mpinzani wake mkuu ni wa chama cha PDP Atiku Abubakar, ambaye pia ametoka eneo la kaskazini.

Wachambuzi wanaeleza uchaguzi huu ni mgumu sana kubashiri, huenda matokeo yakawa yanakaribiana.

Huenda chama cha APC kikapata pigo katika majimbo ya Middle Belt, Benue na Nasarawa, kutokana na kutoridhishwa na kushindwa kukabiliana na ghasia za kieneo, mhariri wa BBC wa Abuja Aliyu Tanko anasema.

APC ina umaarufu katika majimbo mawili yalio na idadi kubwa ya wapiga kura - Lagos na Kano - lakini kuna hatari ya ufuasi sugu na kujitokeza kwa wapiga kura wachache ambayo huenda yakawa ni tatizo.

Ramani za kipato inafichua mgawanyiko wa kieneo katika namna ambavyo raia wa Nigeria walio tajiri walivyo, huku eneo la kaskazini likiwa maskini zaidi kuliko kusini mwa nchi.

Jimbo anakotoka rais Buhari, Katsina kaskazini mwa Nigeria, ni lenye umaskini zaidi , ambako pato jumla la wastani kwa mwaka kwa kila mtu mmoja, ni chini ya $400 (£309) - takriban $1 kwa siku.

Ukiondosha mji mkuu Abuja, Lagos ndio jimbo tajiri na mji mkuu wa biashara ikiwa na kipato jumla kwa wastani kwa mwaka kwa kila mtu mmoja la takriban $8,000.

Utajiri wa jumla kwa majimbo ya kusini, Delta, Bayelsa, Rivers na Akwa Ibom unatokana na biashara ya mafuta.

Takwimu zinaonyesha pato la wastani halidhihirishi tu ni kwa usawa wa kiasi gani fedha zinasambazwa kwa idadi jumla nchini.

Kila mwaka vijana wengi Nigeria wanaanza kutafuta kazi, lakini nafais ni kidoog hususan kazi za ofisini.

Ajira za kudumu ni mojawpao ya changamoto kubwa kwa Nigeria, kwa mujibu wa utafiti wa kampuni ya uhasibu PwC mwaka jana.

Kwa jumla, licha ya matatizo ya hapa na pale, uchumi umekuwa kwa ukubwa tangu mwaka 2000, lakini ukosefu wa ajira unsalia katika kiwango cha juu. Kitaifa upo katika kiwango cha takriban 23%.

La kushangaza ni kwamba licha ya hayo, baadhi ya majimbo, katika eneo la kusini lenye utajiri wa mafuta , yenye kipato cha wastani , pia yanashuhudia ukosefu mkubwa wa ajira . Pamoja na kugusia ukosefu wa usawa wa kipato , hii inaashiria kwamba sekta ya biashara ya mafuta, haitoi nafasi za kutosha za ajira kwa raia wa maeneo hayo.

Average oil price

Opec crude oil price 1960 - 2018

Source:Opec

Biashara ya mafuta na gesi huchangia 9% ya pato jumla la nchi ya Nigeria, lakini fedha inazopata taifa hilo kutokana na biashara hiyo ya mafuta na gesi hujumuisha takriban nusu ya matumizi ya serikali.

Bei ya mafuta duniani, Hivyo basi, ina jukumu kubwa katika kubaini iwapo serikali inaweza kulipa madeni yake.

Nusu ya kwanza ya muhula wa rais Buhari ilikabiliwa na kudorora kwa bei ya mafuta, iliochangia kupanda kwa kasi kubwa deni la serikali .

Usalama ni suala muhimu katika uchaguzi huu huku kukishuhudiwa ghasia za baina ya jamii na zenye mfano wa itikadi kali za dini ya kiislamu zilizosababisha vifo vya takriban watu 10,000 katika miaka minne iliyopita.

Licha ya ufanisi kiasi wa kijeshi tangu 2015, hususan katika kudhibiti upya maeneo yaliodhibitiwa na wafuasi wa Boko Haram katika eneo la kaskazini mashariki, kumeshuhudiwa ongezeko la hivi karibuni la masambulio ya wanamgambo wa kundi hilo.

Katika eneo la kaskazini magharibi, hususan katika jimbo la Zamfara hali inaonekana kuwa mbaya zaidi, huku makundi yaliojihami yakishambulia vijiji na kuwaua na kuwateka raia na kuitisha vikombozi pamoja na wizi wa mifugo.

Mzozo huo wa muda mrefu baina ya wafugaji walioweka makaazi na wafugaji wa kuhama hama umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni hususan Nigeria ya kati. Serikali ya rais Buhari imeshutumiwa kwa usimamizi mbaya wa hali hiyo, lakini kwa sasa inaonekana kuwa mzozo umepungua wakati uchaguzi ukiwadia.

Idadi jumla ya raia nchini Nigeria, milioni 180 imegawanywa kwa idadi ya makundi ya kikabila.

Jamii ya Hausa-Fulani waliopo katika eneo la kaskazini, wengi wao ni waislamu.

Wa Yoruba wa kusini magharibi wamegawanyika kati ya waislamu na wakristu na Igbo wa kusini mashariki na makundi jirani wengi wao ni wakristo au wanafuata imani za kitamaduni.

Wagombea wote wawili wa Urais - Buhari na Abubakar - ni wa kabila la Fulani na wagombea wenza wao wanatoka eneo la kusini. Naibu wa rais Buhari ni Yemi Osinbajo, Mchungaji wa kabila la Yoruba na mhadhiri wa zamani wa sheria; Abubakar upande wake amemchagua Peter Obi, mwanasiasa wa kabila la Igbo.

Kwa mujibu wa shirika la Unicef, moja kati ya watoto watano wasiokwenda shule, ni wa Nigeria- licha ya kwamba asilimia ya watoto walio na umri wa kwenda shule ambao wanapata elimu ina tofautiana katika maeneo tofuati ya nchi hiyo.

Kuna mgawanyiko mkubwa kieneo , huku idadi ya watoto wanaokwenda shule ikiwa chini katika eneo la kaskazini.

Inakadiriwa kwamba watoto milioni 10.5 kati ya umri wa miaka 5 na 14 hawako shuleni.

Mnamo Oktoba mwaka jana, afisa wa Unicef amesema 69% kati yao wako katika eneo la kaskazini mwa Nigeria, na idadi kubwa ikiwa katika jimbo la Bauchi ikifuatwa na anakotoka rais Buhari , jimbo la Katsina.

Baraza la kitaifa la uchumi nchini limependekeza mnamo Oktoba mwaka jana kwamba hali ya hatari itangazwe katika sekta ya elimu kukabiliana na miongoni mwa mambo mengine, idadi ya watoto ambao hawaendi shule.

Viwango vya elimu kwa kawadia viko chini katika eneo la kaskazini, hususan kwa wanawake na wasichana.

Literacy rates

% literacy for 15-24-year-olds

Source: Nigeria National Nutrition and Health Survey 2018

Utafiti wa Christopher Giles, BBC

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii