'Mcheza soka wa kipekee niliyeweka wazi mahusiano yangu ya jinsia moja'
Huwezi kusikiliza tena

Phuti Lekoloane: Mchezaji soka anayebadili mitazamo dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Afrika

Katika mataifa mengi Afrika, ni uhalifu kuwa mpenzi wa jinsia moja, na ni nadra kushuhudiwa wachezaji wanaoweka wazi kuwa wao ni wapenzi wa jinsia moja katika soka. Lakini Phuti Lekoloane analibadili hilo. Anacheza katika daraja la tatu la soka Afrika kusini, na anajaribu kubadili mitazamo ya watu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kutoa nafasi kwa wachezaji zaidi kujitokeza wazi.