Picha halisi ya shambulio katika hoteli ya Nairobi
Huwezi kusikiliza tena

Shambulio la kigaidi Kenya: Yapi yaliojiri wakati wa uvamizi wa hoteli ya DusitD2 Nairobi?

Mnamo Januari 15, watu 21 waliuawa katika shambulio kwenye hoteli ya kifahari na jengo lenye ofisi nyingi katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Shambulio lilidumu kwa saa 19. Lakini nini hasaa kilifanyika kwa wakati huo?

Kwa kutumia mfumo wa 3D, pamoja na ushahidi mpya kutoka kwa manusura, mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama Afrika Tomi Oladipo anawasilisha picha ya kina ya shambulio lilivyotukia siku hiyo, tangu kuanza kwake mpaka muitikio ulioratibiwa na wepesi wa vikosi vya usalama uliookowa maisha ya mamia ya watu.

Video imetengenezwa na: George Wafula, Anthony Irungu, Ben Allen, Anthony Makokha, Hugo Williams, Millicent Wachira, Njoroge Muigai, Gloria Achieng, Ashley Lime na Muthoni Muchiri.

Mada zinazohusiana