Wakenya wahoji taarifa iwapo ni mara ya kwanza chui adimu mweusi ameonekana kwa zaidi ya miaka 100

A male melanistic leopard captured on camera in Africa, for what's thought to be the first time in a century Haki miliki ya picha BURRARD-LUCAS PHOTOGRAPHY

Chui adimu mweusi ameonekana katika eneo la kati nchini Kenya.

Jina 'Black Panther' kama wanavyofahamika chui wengine wa aina hiyo, wamepata umaarufu kutokana na filamu Marekani ambayo inatazamwa pakubwa kote - lakini kupata fursa ya kumuona kwa uhalisi ni kitu adimu sana.

Mpiga picha wa wanyama pori, Will Burrard-Lucas amefanikiwa kumuona - na inadhaniwa kwamba ni mara ya kwanza kwa mtu yoyote kumpiga picha chui wa rangi kama hiyo barani Afrika katika muda wa miaka 100.

Kuna picha chache za kiumbe huyu, ambaye ni wa siri.

Will alipata fununu kuhusu chui huyo mweusi 'Black panther' - neno linalotumika kumaanisga chui mweusi ikitegemea anatokea sehemu gani duniani, - kuwa ameonekana katika kambi ya wanyama pori huko Laikipia.

Baada ya kufuata alama za miguu ya chui huyo katika njia aliyotumia, na kwa usaidizi wa muongozaji wa eneo hilo, Will alijikita sehemu moja alikutundika kamera zake.

"Nimezoea kuweka mitego ya kamera, na huwa mara nyingine sipati chochote, kwasababu ni kama bahati nasibu tu, hujui iwapo mnyama unayetaka kumpiga picha atakuja katika njia ulioweka mtego wako wa kamera."

Walikuwa hawana hakika iwapo njia waliofuata ndio njia iliyofuatwa na chui huyo mweusi au ni chui wa kawaida tu.

"Huwa sina tamaa sana, na baada ya usiku kadhaa, sikumpata chui huyo na nilianza kufikiria, nitakuwa nimepata bahati hata angalau nikapata picha ya chui wa kawaida tu."

Haki miliki ya picha Image copyrightBURRARD-LUCAS PHOTOGRAPHY

Lakini kwa siku wa nne, alibahatika.

Na katika picha zote, chui huyo mweusi alionekana peke yake.

Watafiti wanadokeza kuwa melanin au rangi ya ngozi, ni kinyume cha ulemavu wa ngozi yaani albinism, na mara nyingi hutokea kutokana na jeni inayosababisha kuongezeka kwa kiwango cha rangi mwilini au za manyoya ya mnyama ili kumfanya awe mweusi.

Lakini je hii ni mara ya kwanza kwa mnyama huyo kuonekana au kunakiliwa kuonekana katika miaka 100 kama inavyodaiwa? Wakenya wamelihoji hilo kupitia mitandao ya kijamii:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii