Ma ajenti wa siri wa mauaji Sudan
Huwezi kusikiliza tena

Je ni nini kinafanyika ndani ya vizuizi vya siri Sudan?

Kanda za video zilizopigwa na waandamanaji Sudan zinaonyesha maajenti wa usalama wakiwafukuza waandamanaji, wakiwapiga na kuwaburuza hadi katika vizuizi vya siri.

Ni kina nani walio katika vikosi hivyo vya mauaji, vizuizi hivyo viko wapi, na nini kinafanyika nyuma ya kuta za vizuizi hivyo?

BBC Africa Eye imechambua video kadhaa katika maandamano ya hivi karibuni, na imezungumza na mashahidi walioponea mateso. Baadhi ya waandamanaji wametuambia kuhusu kizuizi cha siri na kinachoogopewa - Jokofu- ambapo baridi inatumika kama chombo cha mateso.

Uchunguzi umeongozwa na: Benjamin Strick, Abdulmoniem Suleiman, Klaas Van Dijken, Aliaume Leroy

Imehaririwa na kutengenezwa na: Suzanne Vanhooymissen, Tom Flannery, Daniel Adamson

Mada zinazohusiana