Wafalme wa nyika, simba wawili, wanyakua tuzo Ulaya

Lions Haki miliki ya picha David Lloyd

Picha ya Simba wawili, iliyopewa jina la Bond of Brothers (urafiki wa ndugu), ndiyo mshindi wa Chagua la Watu katika tuzo za Mpiga Picha Bora wa Wanyama wa Mwaka.

Picha hiyo ilipigwa na David Lloyd, na kuzishinda picha nyengine 45,000 zilizowasilishwa kwenye mchuano huo.

Picha 25 ziliorodheshwa na Makumbusho ya Historia ya Historia ya Asili ili watu wachague wanayoipenda zaidi.

"Nimefurahi sana picha hii kufanya vizuri. Kwa sababu inaonesha hisia za wanyama na kwamba hilo haliishii kwa wanaadamu tu," amesema Lloyd, ambaye ni raia wa New Zealand aliyelowea London.

Picha nyengine zilizopata kura nyingi za watu ni:

Penguins Haki miliki ya picha Wim van den Heever
Image caption 'Penguin Wafalme' watatu katika fukwe ya visiwa vya Falkland iliyopigwa na Wim Van Den Heever.
Urban fox Haki miliki ya picha Matthew Maran
Image caption Mbweha akitembea pembeni ya mchoro wa mbwa jijini London, picha iliyopigwa na Matthew Maran.
Polar bear Haki miliki ya picha Justin-Hofman
Image caption Dubu anayetaabika kwa njaa kaskazini ya Canada, picha iliyopigwa na Justin Hofman
Painted wolves Haki miliki ya picha Bence Mate
Image caption Mbwa mwitu watatu wanaogombea mguu wa swala, picha iliyopigwa na Bence Máté

Picha zote kwa hisani ya Mpiga Picha Bora wa Wanyama wa Mwaka

Mada zinazohusiana