Uchaguzi Nigeria 2019: Changamoto ya kusambaa kwa taarifa ghushi katika mitandao ya kijamii

A crowd at a political rally in Nigeria

Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Nigeria zinatarajiwa kukamilika rasmi leo Alhamisi lakini mitandao ya kijamii imelaumiwa pakubwa kwa kuchangia kusambaa kwa taarifa za kughushi.

Vyama vyote vikuu vya kisaiasa vimeiambia BBC kuwa wapinzani wao walihusika na kusambazwa kwa habari hizo.

Rais Muhammadu Buhari, anayegombea muhula wa pili madarakani kwa tikiti ya chama cha Progressives Congress (APC), na mpinzani wake mkuu Atiku Abubakar, wa chama cha People's Democratic Party (PDP), wameshambuliwa kwenye video zilizo na taarifa za ghushi katika mitandao ya kijamii.

"Kampeni za chama cha PDP zimekuwa zikitumia mbinu ya kusambaza taari za uwongo ili kuwapotosha watu," anasema Tolu Ogunlesi, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya dijitali wa rais Buhari.

Vyama vyote viwili vimenasema havina ufahamu kuhusu watu wanaosambaza taarifa za uwongo ndani ya vyama vyao.

"Chama cha APC kinaendesha taarifa za propaganda - kiasi cha kufanyia ukarabariti picha na maneno kufikia lengo lao," anasema Paul Ibe, mshauri wa mawasiliano wa Bw. Atiku Abubakar.

Madai ambayo chama cha APC imepinga vikali huku ikiilaumu PDP kwa kusambaza taarifa za ghushi.

Kitengo cha BBC Reality Check kimekusanya baadhi ya taarifa ghushi zilizotolewa dhidi ya wagombea wawili wakuu wa urais katika uchaguzi wa Nigeria.

Maelezo ya picha,

Wasichana wa Dapchi walisafirishwa hadi Abuja kwandege ya kijeshi

Kutoweka kwa wasichana wa Dapchi

Taarifa ghushi zilianza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii siku chache kumhusu msichana Leah Sharibu, wa miaka 15 aliyekuwa ametekwa na wanamgambo wa Boko Haram kwa kukataa kujiunga na na dini ya Kiislam

Zaidi ya wasichana 100 walitekwa kutoka kijiji cha Dapchi, Kaskazini mwa Nigeria, lakini wote waliachiliwa.

Taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya WhatsApp na Facebook, zilidai kuwa Leah amefariki - nalilisambaa kwa kasi sana mitandaoni.

Mtu asiyejulikana na aliyedaiwa kuwa "jamaa wake" alithibitisha kifo cha msichana huyo, kwa mujibu wa taarika kwenye mitandao ya kijamii.

Kujibu madai hayo serikali ilitaja kuwa ''Taarifa feki'' na bw. Ogunlesi, kutoka kampeni ya rais Buhari anasema taarifa hiyo ilitumika dhidi ya serikali.

Pesa za bure?

Taarifa nyingine inahusiana na madai kuwa mgombea wa upinzani Atiku Abubakar alipanga njama ya kupeana pesa na chakula katika moja ya kampeni zake.

Taarifa hii iliwekwa mtandaoni na msaidizi wa rais Buhari, aliyeweka picha ya vyombo vya chakula vilivyofungwa kwa kutumia sarafu ya noti ya Nigeria katika jimbo la Sokoto.

"Wafanye masikini, kisha wahonge kwa pesa - Atiku alisema hayo jana mjini," aliandika.

Kampeni ya Buhari imekanusha kuhusika na taarifa hiyo.

Ilibainika kuwa picha hiyo ilipigwa mika miwili iliyopita katika hafla ya wakfu wa Kokun dhidi ya Njaa.

Mshauri wa kampeni ya Atiku ameiambia BBC Reality Check: "Atiku hawezi kumpatia hongo mtu yeyote."

Kuididimiza zaidi Nigeria?

Video nyingine ni ile inayodai Atiku Abubakar amefikia mkataba na Boko Haram kwa kuwapa ardhi na mafuta.

Video hiyo ilitizamwa zaidi ya mara 200,000, ilisambazwa na kundi linalojiita ''Make Nigeria Worse Again''.

Lakini haina maelezo kuhusi ni lini na wapi kampeni ya Atiku ilitangaza mpango huo.

Maafisa wa kampeni ya Atiku wameiambia BBC Reality Check kwamba hawana mpango wowowte kama huo - "hakuna kitu kama hicho".

Buhari alipopiga kura 'dhidi ya Nigeria'

Taarifa nyingine ya uwongo inayosambazwa mitandaoni ni ile inayodai kuwa Muhammadu Buhari alikuwa akiwapendelea watu wa jamii yake alipokuwa mkuu wa majeshi miaka ya 1980.

Taarifa hiyo inahusiana na hatua ya bw. Buhari kutomuunga mkono mgombea wa Nigeria katika wadhifa wa katibu mkuu Muungano wa Afrika.

Badala ya kuangazia kwanini aliamua kuchukua hatua hiyo, taarifa iligeuzwa kuwa alimuungha mkono mgombea wa nchi jirani ya Niger

Taarifa hiyo ilipingwa vikali na msemaji wa rais, Garba Shehu.