Wapenzi wa jinsia moja Japan wafungua kesi ya kudai haki ya kuoana

Ai Nakajima and Tina Baumann
Maelezo ya picha,

Ai Nakajima and Tina Baumann are married in Germany, but Japan doesn't recognise that

Wapenzi 13 wa jinsia moja nchini Japan wameenda mahakamani hii leo wakidai haki ya kuoana.

Katika madai yao, wanasema kukataza ndoa hizo ni kuvunja haki yao ya kikatiba.

Endapo mahakama za nchi hiyo zitakubaliana nao, ndoa hizo zitakubalika rasmi nchini humo.

Japan ndiyo nchi pekee miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani (G7) ambayo haijaruhusu ndoa hizo, lakini tafiti zinaonesha kuwa vijana wanakubaliana nazo.

'Jamii ya kihafidhina'

Wapenzi hao wa jinsia moja watafungua kesi katika miji tofauti ya nchi hiyo katika siku ya wapendanao (Valentine's Day).

Ai Nakajima, 40, kutoka Japan, na mpenzi wake Tina Baumann, 31, kutoka Ujerumani ni miongoni mwao.

Wawili hao wapo pamoja toka mwaka 2011 walipokutana jijini Berlin. Baada ya kuishi pamoja Ujerumani kwa miaka kadhaa, waliamua kuhamia Japan.

Maelezo ya picha,

The two say life as a gay couple is very different in Germany and Japan

Lakini maisha ya wapenzi wa jinsia moja ni tofauti kabisa katika nchi hizo.

"Jamii ya Wajapani kwa asili ni ya kihafidhina," bi Nakajima ameiambia BBC.

Wengi wa rafiki zao wanashindwa kujitokeza mbele ya jamaa zao na kujitangaza kuwa ni wapenzi wa jinsia moja.

Japo Japan ni nchi ya kitamaduni, tafiti zinaonesha kuwa vijana wengi hawana mtazamo hasi na ndoa za jinsia moja.

Kuanzia mwaka 2015, baadhi ya miji imeanza kutoa vyeti kwa wanandoa wa jinsia moja, lakini vyeti hivyo havitambuliki kisheria.

"Japo kuna uungwaji mkono kutoka kwa vijana, wanasiasa wengi ni watu wazima na ni wagumu kubadili mambo," amesema bi Nakajima na kuongeza; "tumejipanga kulipeleka suala hili mpaka mahakama ya juu zaidi. Tukitumia njia hiyo itatuchukua mpaka miaka mitano."

Maelezo ya picha,

Mwaka 2015 mji wa Shibuya ulikuwa wa kwanza kutoa cheti kwa wanandoa wa jinsia moja Japan

Safari ndefu

Katiba ya japani inasema "ndoa inabidi ipate ridhaa ya pande zote mbili za jinsia" na mamlaka imekuwa ikitafsiri kipengele hicho kama katazo kwa ndoa za jinsia moja.

Lakini wanasheria wa wapenzi hao wa jinsia moja wanadai kuwa kipengele hicho kimewekwa ili kuzuia ndoa za kulazimishwa.

Kesi za Alhamisi ya leo kwa vyovyote vile ni sehemu ya kwanza tu ya safari ndefu, lakini wanaharakati wamesema wapo tayari kwa mapambano yatakayochukua muda mrefu alimradi ndoa hizo zinapitishwa nchini mwao.