IAAF limekana kuiambia mahakama kuwa wanariadha kama Caster Semenya watazamwe kama wanaume

South Africa's Caster Semenya celebrates victory following the Womens 800 Metres during day two of the IAAF Continental Cup in Czech Republic Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Caster Semenya ndiye bingwa mara mbili wa Olimpiki na bingwa mara tatu wa dunia wa mbio za mita 800

Shirikisho la riadha duniani IAAF limekana kwamba litaiambia mahakama kuwa wanariadha wote wanawake wenye viwango vikubwa vya homoni za kiume mwilini, yaani testosterone kama vile Caster Semenya wanapaswa kutambuliwa kama wanaume.

Bingwa wa dunia na Olimpiki katika mbio za mita 800 anapinga sheria iliyopendekezwa na IAAF inayonuiwa kudhibiti viwango vya homoni hiyo kwa wanariadha wanawake.

Kesi hiyo itasikilizwa katika mahakama ya malalamiko katika michezo (Cas) wiki ijayo.

Gazeti la the Times limeripoti kuwa mawakili wa IAAF watasema kuwa Semenya "kibayolojia ni mwanamume" pamoja na kwamba anatambuliwa kuwa mwanamke.

Shirikisho hilo la riadha linasema "halitambui" mwanariadha yoyote mwenye "tofuati za kukuwa kijinsia" (DSD) - ambapo raia wa Afrika kusini, Semenya ndiye anayeonekana zaidi - kuwa mwanamume .

"Kinyume na hicho, tunakubali jinsia zao kisheria pasi na shaka, na tunawaruhusu washiriki katika kitengo cha wanawake," lilisema siku ya Jumatano.

"Hatahivyo, iwapo mwanariadha aliye na hali hiyo ya DSD, atakuwa na sehemu nyeti za kiume, na viwango vya kiume vya homoni hiyo ya testosterone, wanpaata ongezeko la mifupa na uzito wa misuli na nguvu na huongeza damu mwilini ambayo mwanamume hupata wanapo baleghe, ndicho kinachowapatia wanaume nguvu zaidi ya wanawake katika mashindano.

"Kwahivyo, ili kuwa na ushindani wa sawa katika kitengo cha wanawake, ni muhimu kuwataka wanariadha walio na hali ya DSD kuzipunguza homoni kusalia kuwa kama za wanawake kabla hawajaruhusiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa"

IAAF ilinuia kuuidhinihsa sheria mpya mnamo Novemba 1 mwaka jana lakini ikaahirisha hadi Machi 26 kusubiri matokeo ya kesi aliowasilisha Semenya na shirikisho la riadha Afrika kusini.

Kuahirishwa huko kunamaanisha kuwa wanariadha wenye hali hiyo ya DSD hawatoruhusiwa kushiriki katika mashindano kwa miezi 6 kutoka tarehe ambayo mabadiliko ya sheria yataidhinishwa ambayo, huenda ikamfanya Semenya akakosa kushiriki baadhi ya mashindano ya msimu wa nje 2019.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mashindano ya ubingwa wa riadha 2019 yanaanza mjini Doha Septemba 27.

Wakati Semenya, alipotangaza kwamba atapambana na sheria hizo mwaka jana Afrika kusini alisema: "Sio haki. Nataka nikimbie kama kawaida, namna nilivyozaliwa

"Mimi ni Mokgadi Caster Semenya. Mimi ni mwanamke na nina kasi."

Katrina Karkazis, mtafiti mkuu mwenza katika chuo kikuu cha Yale, na mtaalamu mkuu wa masuala ya homoni hiyo ya testosterone, ni miongoni mwa walioshutumu shirikisho hilo la riadha duniani kuhusu msimamo wake.

Amesema IAAF "inatafasiri vibaya sayansi ya bayolojia ya jinsia" na inatafuta "kuunda ufafanuzi wake binafsi wa jinsia kutokana na imani zenye makosa kuhusu bayolojia na jinsia.".

Ameeleza kwamba hilo halina msingi na linaweza kuwa na madhara zaidi kwa kuidhinihsa ukosefu wa uelewa na kuchangia unyanyasaji zaidi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii