Muhammadu Buhari, kiongozi wa Nigeria anayepigwa vita

Muhammadu Buhari, rais wa Nigeria Haki miliki ya picha AFP

Huku rais wa Nigeria akiwania muhula wa pili wa urais, atalazimika kutotumia ajenda yake iliomsaidia kushinda uchaguzi uliopita wa ahadi ya kuwa na mwanzo mpya.

Wakati huo alikuwa akionyesha fagio jipya, nembo ya chama chake.

Alikuwa hajachaguliwa kidemokrasia licha ya kujaribu mara tatu na sura yake kama mtu asiye mfisadi na mwenye nidhamu ilijitokeza alipokuwa kiongozi wa jeshi katika kipindi cha miezi 20 miaka ya 80.

Alifanya kampeni kama mwanademokrasia mpya , akiapa kukabiliana na ufisadi, kufufua uchumi na kuwashinda wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Wapiga kura waliochoka na ufisadi , ukosefu wa usalama na uchumi mbaya waliamini maneno yake na kumfanya kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani aliyeibuka mshindi dhidi ya raia aliyekuwa madarakani.

Ushindi wa Bwana Buhari 2015 haukuwa tu dhihirisho la kupendwa kwake bali pia kupiga msumari wa mwisho siasa za jadi.

Rekodi yake katika ofisi

Wakosoaji wa bwana Buhari wanasema kuwa misimamo iliowavutia watu na kumpigia kura ndio imeonekana kuwa mambo yanayomgeukia.

Wanamshutumu kwa kuwa dikteta mbali na kushindwa kuwepo uongozini.

Alichukua miezi sita kuchagua baraza lake la mawaziri na amejipatia jina la utani "Baba-Go-Slow".

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mgombea mwenza wa rais Buhari, Yemi Osinbajo kulia

Wafuasi wa Bwana Buhari wanahoji kwamba ametimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni kama vile kukabiliana na ufisadi na kukabiliana na kundi la Boko haram.

Lakini wameshindwa kuonyesha mambo aliyotimiza katika sekta nyengine kama vile kuimarisha uchumi.

Uchumi wa taifa hilo ulianguka wakati alipokwua madarakani, kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.

Tatizo hilo pia huenda lilisababishwa na hatua ya rais Buhari kupinga kushusha thamani ya Naira swala lililochangia upungufu wa sarafu ya Naira katika mwaka wa kwanza wa uongozi wake.

Kampuni ambazo zilifaa kuingiza bidhaa na vifaa zililazimika kutegemea soko la magendo kupitia dola ya Marekani .

Ukosefu wa ajira uliongezeka maradufu hususan kutokana na takwimu za kuhuzunisha katika taifa ambalo thuluthi mbili ya idadi ya watu ni masikini.

Kutokana na hilo , raia wengi wa Nigeria watataja muhula wa kwanza wa rais Buhari kama wakati ambapo matatizo yao ya kifedha yaliongezeka huku hali yao ya maisha ikidorora.

Ajenda yake ya kutaka kuchaguliwa kwa muhula wa pili itategemea na maoni ya raia kwamba ni yeye wa kulaumiwa kwa hali ngumu ya maisha inayowakabili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Buhari ni maarufu miongoni mwa raia wa Nigeria wanaoishi kaskazini ma taifa hilo.

Lakini kwa upande mwengine raia huyo aliimarisha uwekezaji katika miradi ya kilimo pamoja na ile ya ujenzi wa miundo mbinu, mbali na kusimamia uzalishaji wa mafuta zaidi kusini mwa taifa hilo.

Pia anaweza kujigamba kwa kusaidia taifa hilo kujikwamua katika uchumi uliokuwa umeanguka , ijapokuwa kupanda kwa bei ya mafuta duniani huenda kulishinikiza pakubwa na kuimarika kwake kumekuwa kwa polepole sana.

Utawala wa rais Buhari umekumbwa na maswali mengi kuhusu hali yake ya kiafya. Tangu 2017 , rais amekuwa nje ya taifa hilo , akipokea matibabu .

Huku rais huyo mwenye umri wa miaka 76 akikataa kutaja ni nini haswa kinachoathiri afya yake, alikana kwamba alikuwa amekodisha mwili kama wake kumwakilisha katika mikutano ya hadhara.

Umaarufu wake unatokana na watu masikini kaskazini mwa Nigeria wanaojulikana kama 'talakawa', kwa lugha ya Kihausa.

Katika uchaguzi uliopita, ombi lake nchini humo lilipigwa jeki kwa kuwaunga watu maarufu waliokihama chama cha tawala .

Wakati huu, tegemeo lake kubwa ni mgombea mwenza Yemi Osinbajo, muubiri maarufu kutoka eneo lenye Wakristo wengi la kusini mwa Nigeria.


Mtu mwenye nidhamu

Haki miliki ya picha AFP
  • Alizaliwa 1942 katika familia ya Kiislamu katika jimbo la kaskazini la Katsina
  • Akiwa mwanajeshi wa zamani , aliongoza utawala wa kijeshi wa 1980, anakumbukwa kwa ukali wake kwa wafanyikazi wazembe wa serikali ambao walilazimika kuruka kama vyura hadharani.
  • Alishinda uchaguzi wa urais wa 2015 , akiwa mgombea wa kwanza wa upinzani kufanikiwa kumshinda rais aliyepo madarakani baada ya kuahidi kukabiliana na Boko haram na kumaliza ufisadi.
  • Alimwambia mkewe kwamba anafaa kuwa jikoni baada ya kulalamika kuhusu mahojiano na BBC
  • Baada ya kutoweka kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa alilazimika kukana uvumi kwamba mahala pake palikuchukiliwa na mtu anayefanana naye.

Miongoni mwa mambo ambayo alifanikiwa kutekeleza: anaweza kujigamba kwa kuimarisha usalama kaskazini masharki mwa taifa hilo.

Chini ya uongozi wake , jeshi la Nigeria lilifanikiwa kuyakomboa maeneo ambayo yalikuwa yametekwa na wapiganaji wa Boko haram ambao walikuwa wakipigana kuipindua serikali na kuanzisha serikali ya Kiislamu.

Wasichana wengi wa shule ambao walikuwa miongoni mwa kundi la wasichana wa shule wapatao 300 waliotekwa na kundi la Boko haram pia wamekutanishwa na wazazi wao.

Hatahivyo, wengi wa wale waliotajwa kuwa Chibok Girls bado hawajulikani waliko, na mashambulio ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Boko Haram wamerejesha nyuma hatua za kuimarisha usalama ambazo zilikuwa zimeafikiwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wengi wa wasichana wa Chibok waliotekwa nyara na Boko Haram wamekutanishwa ana familia zao

Kulingana na Andrew Walker, mchanganuzi wa Nigeria ambaye ameandika kitabu kuhusu Boko Haram , kundi hilo la wapiganaji lina rekodi ya kunyamaza kwa kipindi kirefu kabla ya kuungana tena na kutekeleza uvamizi .

''Bwana Buhari alionekana kufanikiwa kunyamazisha Boko haram kwa kipindi kirefu ambacho kinaonekana kuisha'', anasema.

Uaminifu wa kibinafsi

Tatizo la kitendo cha usalama cha Nigeria sio tu katika eneo la kaskaizni mashariki.

Jimbo lenye umasikini mkubwa la kaskazini magharibi la Zamfara limekumbwa na visa vingi vya utekaji nyara na mauaji yanayohusishwa na magenge ya wizi wa ng'ombe pamoja na yale makundi ya kuweka usalama mitaani.

Ghasia pia zimeenea katika maeneo mengine yenye historia ya ukabila na mizozo ya kidini.

Majeshi yalilazimika kupelekwa katika majimbo ya kati baada ya ghasia mbaya kati ya wakulima na wafugaji wa kabila la Fulani.

Wakati huohuo kundi la watu wa Biafra wanaotaka kujitenga wameanzisha upya juhudi zao

Baada ya kipindi cha miaka minne cha uongozi wa rais Buhari, bwana Walker anasema: Raia wengi wa Nigeria wanauliza iwapo uaminifu pekee unatosha kuimarisha uadilifu wa taifa hilo.

Ajenda ya Bwana Buhari kutokubali ufisadi imemfanya kumaliza muhula wake wa kwanza ikiwa ni swala gumu miongoni mwa viongozi wa Nigeria.

Hatahivyo ameshutumiwa kwa kutumia uchunguzi wa ufisadi kama kifaa cha kuwanyamazisha wapinzani wake wa kisiasa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hatua ya Buhari ya kumfuta jaji mkuu ilizua hisia kali

Mnamo mwezi Januari 2019, Buhari alimsimamisha kazi kwa muda jaji mkuu nchini humo Walter Onnoghen, kuhusiana na kushindwa kwake kutangaza mali yake kabla ya kuchukua hatamu 2017.

Hatua hiyo iliochukuliwa wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu ilizua hisia.

Kama wakili mkuu wa taifa , jaji Onnoghen angechukua jukumu muhimu la kuangazia migogoro muhimu ya uchaguzi.

Hatahivyo bwana Buhari alikana madai yaliowasilishwa na wachunguzi wa kigeni na wanasiasa wa upinzani kwamba hatua hiyo ilichangiwa na uchaguzi unaotarajiwa.

Pingamizi ya uongozi wa bwana Buhari pia imekumba chama chake cha All Progressives Congress (APC).

Mwaka 2018, chama hicho kilidhoofishwa na misururu ya wanachama kuhamia vyama vingine huku wabunge wengi wakijiunga na chama cha PDP.

Kulikuwa na ishara kwamba mambo hayakuwa mazuri mwaka 2016 , wakati mkewe rais aliambia BBC kwamba maafisa wachache walikuwa wameuteka nyara utawala wa mumewe wakichukua jukumu la kuwateua maafisa wa serikali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aisha Buhariamekua mkosoaji mkubwa wa uongozi wa mumewe.

Shambulio hilo kutoka kwa mtu wa karibu halikutarajiwa na lilikuwa baya kwa kiongozi ambaye alikuwa ameapa kukabiliana na upendeleo.

Bwana Buhari alijibu ukosoaji huo kwa kusema kuwa mkewe anafaa kuwa jikoni jibu ambalo halikuifurajhisha jamii ya kimataifa.

Akiwa mwanajeshi

Bwana Buhari alizaliwa 1942, kwa familia kubwa ya Kiislamu katika jimbo la kaskazini la Katsina .

Katika mahojiano ya mwaka 2012, alitaja kumbukumbu zake za kutupwa kutoka juu ya farasi na babake na nduguye wa kambo.

Baada kukamilisha masomo ya shule , alijiunga na shule ya mafunzo ya kijeshi , akajiunga na jeshi la Nigeria muda mfupi baada ya taifa kujipatia uhuru kutoka Uingereza.

Miaka kadhaa baadaye alisifu nidhamu yake kutokana na shule aliyokwenda na hatua yake ya kujiunga na jeshi akisema kuwa taasisi hizo mbili zilimpatia mafunzo muhimu ya kuwa na bidii.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jenerali Buhari alihudumu miezi 20 kama kiongozi wa kijeshi wa Nigeria mika ya 80.

Mwaka 1983, alikuwa kiongozi wa taifa kufuatia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Shehu Shagari.

Bwana Buhari baadaye alikana jukumu lake katika mapiduzi hayo akisisitiza kuwa uwezo mkubwa upo na waliopanga mapinduzi hayo lakini wazo hilo lilipingwa.

Utawala wake utakumbukwa kwa kampeni yake dhidi ya ukosefu wa nidhamu na ufisadi , pamoja na unyanyasaji wa haki za binaadamu wa mamia ya watu ikiwemo wanasiasa , wafanyibiashara na waandishi wa habari walifungwa jela chini ya sheria kandamizi.

Utawala wake pia ulimfungia mwanamuziki mashuhuri wa Nigeria fela Kuti kutokana na madia ya usafirishaji wa sarafu ya Nigeria nje ya taifa hilo.

Hatua ya utawala wake kukabiliana na bidhaa zinazoingizwa nchini humo ulisababisha kupungua kwa ajira na sarafu mpya ilizinduliwa katika juhudi za kukabiliana na ufisadi.

Bei ya vitu ilipanda , viwango vya maisha vilishuka na baada ya miezi 20 , Bwana Buhari alipinduliwa katika mapinduzi mengine yalioongozwa na mkuu wa jeshi jenerali Ibrahim Babangida.

Bwana Buhari alifunga ndoa mara mbili i , kwanza alimuoa mkewe wa kwanza Safinatu Yusuf, na baadaye Aisha Halilu.

Ana watoto 10.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii