Jussie Smollett: Nyota wa filamu ya Empire 'aliyedaiwa kuwalipa ndugu 2 wa Nigeria kumshambulia'

smollett Haki miliki ya picha AFP

Maafisa wa polisi wa mjini Chicago wanaamini kwamba nyota wa filamu ya Empire Jussie Smollett huenda 'aliwalipa' watu wawili mwezi uliopita kumshambulia, kulingana na ripoti nchini Marekani.

Ndugu wawili raia wa Nigeria ambao walishiriki katika filamu hiyo ya Empire waliambia maafisa wa polisi kwamba walilipwa ili kushiriki katika shambulio hilo la Januari 29, kulingana na vyanzo vya polisi.

Smollett anasema kuwa alishambuliwa na wanaume wawili weupe.

Mawakili wake wamekana hilo kwamba alishiriki katika kupanga shambulio hilo la kiubaguzi wa rangi.

'Hakuna ukweli wowote na mtu anayedai uvumi huo ni muongo', ilisema taarifa.

Taarifa hiyo inasema kuwa mmoja ya ndugu hao alikuwa akifanya kazi kama mkufunzi wa kibinafsi wa Smollett.

Ola na Abel Osundairo wote walishiriki katika filamu hiyo.

Katika chapisho hili la instagram , Ola Osundairo kulia anaonekana na mwanzilishi wa Empire Lee Daniels katikati.

Je ni yapi mapya?

Raia hao wa Nigeria walio na umri wa miaka 25 na 27, waliondoka nchini Marekani baada ya shambulio hilo la Januari 29 .

Walikamatwa walipokuwa wakirudi mnamo Jumatano lakini wakaachiliwa siku ya Ijumaa na sasa wanadaiwa kushirikiana na maafisa wa poilisi.

Siku ya Jumamosi maafisa wa polisi wa Chicago walisema kuwa uchunguzi kuhusu shambulio hilo 'umebadilika' kufuatia madai ya awali kwamba shambulio hilo lilikuwa limepangwa.

Haki miliki ya picha Chicago Police
Image caption Maafisa wa polisi wa Chicago walitoa kanda ya video ya watu wawili katika kesi hiyo.

Raia hao wa Nigeria wanasema kuwa walinunua kamba hiyo iliotumika katika shambulio hilo katika duka moja , maafisa wa polisi waliambia vyombo vya habari nchini Marekani.

Polisi waliokuwa wakipekuapekua nyumba wanayoishi walipata kamba , barakoa na dawa ya klorini.

Je Smollett amesema nini?

Smollett amesema kuwa washambuliaji hao walimtukana kwa kutumia maneno ya kibaguzi walipokuwa wakimpiga kabla ya kumwagia kemikali fulani na kumwekea kamba shingoni mwake.

"Hili ni taifa la Maga," anasema walimwambia , wakitaja kauli mbiyu ya Donald Trump Make America Great Again .

Msanii huyo anasema kuwa 'ambebadilishwa kabisa' na kisa hicho.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii