Britam Towers: Jumba refu zaidi Afrika mashariki na kati lashinda tuzo Ujerumani

Jumbe refu zaidi Afrika mashariki na kati

Jumba refu la Britam Tower lililopo jijini Nairobi nchini Kenya limepokea tuzo inayopewa majumba marefu duniani ya Emporis Skyscraper Award.

Ni jumba la pekee barani Afrika kushiriki katika tuzo hiyo miongoni mwa majumba 10 bora duniani katika historia ya tuzo hiyo ya miaka kumi na tisa.

Hatua hiyo inalifanya jumba hilo lililojengwa na kampuni ya Britam Properties Limited kuwa jumba refu zaidi katika eneo la Afrika mashariki na kati , likiwa na urefu wa mita 200.

Britam Tower lilichunguzwa pamoja na mengine mengi barani Ulaya, Asia na Marekani ambayo yalishirikisha Generali Tower mjini Milan, jumba la Chicago's 150 North Riverside na lile la Riverpoint.

Haki miliki ya picha Chung Sung-Jun

Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na jumba la Lotte World Tower mjini Seoul, Korea Kusini. Tuzo ya The Emporis Skyscraper ni tuzo maarufu duniani miongoni mwa ujenzi wa majumba marefu.

Washindi huchaguliwa na jopo la wataalam wa usanifu kutoka kila pembe duniani , huku majumba yelioteuliwa kuwania tuzo hiyo yakishinda kwa vigezo vya mvuto na ufanisi wao.

Likiwa katika eneo la Upper hill jijini Nairobi jumba hilo lenye ghorofa 31 linatoa mandhari ya kupendeza ambapo unaweza kuona eneo la kati la mji mkuu wa Nairobi pamoja na maeneo ya viungani mwake ikiwemo mbuga ya wanyama pori ya Nairobi.

Ujenzi wake ulikamilika mnamo mwezi Novemba 2017, na sasa linamilikiwa na kampuni ya bima ya Britam Life Assurance Limited.

Katika siku nzuri isio na mawingu unaweza kuona Mt. Kilimanjaro pamoja na Mt Kenya juu ya jumba hilo.

Haki miliki ya picha Antoine Antoniol

Majumba mengine marefu duniani ni Eiffel Tower lililopo mjini Paris ambalo halijafikia urefu wa mita 300, Jumba la Time Warner lililopo mjini New York na lenye urefu wa mita 200 na lile la Gherkin mjini London lenye urefu wa mita 180.

Image caption Jumba la UAP jijini Nairobi

Awali Jumba la UAP Old Mutual jijini Nairobi ndio lililokuwa likishikilia nafasi ya jumba refu zaidi katika eneo la Afrika ya mashariki likiwa na ghorofa 33 na urefu wa mita 163.

Lilikuwa linafuatiwa katika orodha hiyo na Jumba la Twin Tower mjini Dar es salaam lenye ghorofa 35 na urefu wa mita 153.

Hatahivyo Kenya inatarajiwa kumiliki jumba refu zaifdi barani Afrika baada ya rais Uhuru Kenyatta kuweka jiwe la msingi la Jumba la Pinnacle Tower .

Haki miliki ya picha IKULU YA RAIS NAIROB
Image caption Picha ya eneo litakalojengwa jumba refu zaidi barani Afrika

Jengo hilo litakalojengwa katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi, litakuwa na ghorofa 70 na urefu wa futi 900 hivyobasi kulifanya kuwa refu zaidi barani.

Jumba hilo litakuwa na ofisi za kibiashara nyumba za kukodisha na Hoteli ya Hilton Hotel mbali na kuwa na duka la jumla na kituo cha burudani.

Kwa sasa jumbe refu zaidi barani Afrika ni lile la Carlton Center lililopo mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Limekuwa jumba refu zaidi kwa kipindi cha miaka 39 .

Jumba la Pinnacle Towers nchini Kenya litakuwa miongoni mwa majumba marefu duniani.

Dubai Burj Khalifa ndio jumba refu zaidi duniani likiwa na urefu wa mita 800.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii