Jinsi hesabu zilivyoijenga China na kumwezesha Mfalme 'kulala' na wanawake 121 dani ya siku 15

The Forbidden City in Beijing Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption When Greece declined, mathematical progress in China achieved new heights

Kuanzia kupiga hesabu ya nyakati mpaka kuvuka bahari, hesabu ndio utaalamu ambao falme na ustaarabu wa watu wa kale waliutegemea.

Safari ya uvumbuzi wa hesabu ilianzia Misri, kisha Mesopotamia na Ugiriki, lakini baada ya dola hizo kuanguka, maendeleo ya hesabu nayo yakaanguka ka umande wa Magharibi.

Lakini kwa upande wa Mashariki mambo yalikuwa tofauti na hatua kubwa zilikuwa zikipigwa.

China ya kale, hesabu ndio kilikuwa kiungo tegemezi cha kusimamisha Ukuta Mkuu ambao mpaka leo ni moja ya maajabu ya dunia.

Na namba zilikuwa muhimu hata katika kupangilia maisha katika nyumba ya ufalme.

Mpangilio wa hesabu za mapenzi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kuwa mfalme kulihitaji mtu awe na nguvu za kutosha

Kalenda na mwenendo wa sayari ndio vilichangia maamuzi yote ya mfalme, mpaka namna maisha yake ya mchana - na usiku - yalivyopangiliwa.

Washauri wa mfalme walitengeneza mfumo ambao ulimuwezesha mfalme kulala na idadi kubwa ya wanawake walokuwa chini ya milki yake.

Mfumo hou wa kijiometriki, ulimuwezesha kulala na wanawake 121 ndani ya siku 15 tu, ambao ni;

  • Malkia
  • Wapenzi wakuu 3
  • Wake 9
  • Wake wadogo 27
  • Watumwa 81.

Kila kundi ni kubwa mara tatu zaidi ya kundi la awali. Kutokana na mfumo huo, wataalamu wa hesabu walimuwezesha mfalme kuwa na kalenda ambayo ilimfikia kila mwanamke aliyekuwa katika milki yake.

Nguvu ya mfalme

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Si nyumba ya mfalme tu ndio ambayo ilitegemea hesabu, bali mambo yote ya utawala wa nchi.

Usiku wa kwanza ulitegwa maalumu kwa malkia. Usiku wa pili kwa wapenzi wake wakuu watatu. Wakeze tisa usiku wa tatu, baada ya hapo wakeze wadogo 27 walilala nae kwa siku tatu tisa kwa usiku mmoja.

Baada ya hapo katika kipindi cha siku 9 zilizofuata, watumwa 9 tofauti walikuwa wakilala na mfalme kila siku.

Mfumo huo uliwekwa maalumu ili wanawake wenye wadifa mkubwa zaidi walale nae katika kipindi ambacho mwezi huangaza zaidi, kipindi ambcho yin au nguvu zao zipo katika kiwango cha juu ili zikabiliane na yan au nguvu za mfalme za kiume.

Kuwa mfalme kulihitaji mtu awe na nguvu za kutosha, lakini malengo yalikuwa wazi - kuzaa wanamfalme wengi inwezekavyo ili kuwezesha ufalme uendelee.

Si nyumba ya mfalme tu ndio ambayo ilitegemea hesabu, bali mambo yote ya utawala wa nchi.

Kuvutiwa na hisabati

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption China ya kale ilikuwa na eneo kubwa ambalo lilitawaliwa kwa sheria kali, zikiwemo za kodi, vipimo vya uzani na pesa.

China ya kale ilikuwa na eneo kubwa ambalo lilitawaliwa kwa sheria kali, zikiwemo za kodi, vipimo vya uzani na pesa.

Dola hiyo ilikuwa ikitumia mfumo wa desimali miaka 1000 kabla ya nchi za Magharibi kuanza kutumia. Wachina walikuwa wanamifumo ya hisabati ambayo haikuonekana katika nchi za Magharibi mpaka mwanzoni mwa karne ya 19.

Kulingana na ngano za kale, mtawala wa kwanza wa China aitwaye Mfalme wa Njano, alitengezewa hisabati na moja ya miungu yake mwaka 2800 kabla ya kuzaliwa Kristo akiamini kuwa fani hiyo ina nguvu kubwa.

Mpaka leo, Wachina wanaamini katika nguvu hizo za ajabu za nambari.

Namba tasa zinachukuliwa kuwa ni za kiume na shufwa ni za kike.

Namba nne huepukwa na nguvu zote, wakati namba nane huleta bahati nzuri.

Mada zinazohusiana