Uchaguzi Nigeria: Buhari kuwaonya wezi wa Kura

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Maelezo ya picha,

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema ameamuru Polisi na wanajeshi kutowahurumia watu watakaobainika na wizi wa kura katika kipindi hiki cha kuelekea upigaji wa kura wa taifa hilo,

kufuatia kusogezwa mbele kwa wiki moja uchaguzi huo.

Hata hivyo Buhari na upande upinzani kwa pamoja waliikosoa tume kwa kuahirisha upigaji kura na kudai kuwa tume hiyo inamapungufu na kutaka uchunguzi ufanywe.

Chanzo cha picha, Reuters

Hata hivyo wakosoaji wa kisiasa nchini Nigeria wamepokea tofauti kauli hiyo ya Rais Buhari,wakidai kuwa yeye pia ni miongoni mwa wezi wa kura.

Tume ya uchaguzi ya Nigeria pamoja kukosolewa wamejitetea kwamba hatua yao ya kusogeza mbele uchaguzi ilitokana na ugumu wa usambazi wa vifaa kufuatia eneo kuwa kubwa.

Kauli hiyo ya Rais anayemaliza muda wake Buhari,imetolewa katika mkutano wa chama chake wa dharula uliofanyika mjini Abuja.

Akizungumza kwa msisitizo Buhari amesema kwa yeyote atakaye fanya jaribiop la udanganyifu au fuje awe tayari kulipa gharama ikibidi ya uhai wake.

Chama kikuu cha upinzania nchini Nigeria PDP kimesema kauli ya Buhari ni sawa na kutoa kibali cha mauaji kwa raia wake.

Mashaka juu ya kuhairishwa kwa uchaguzi

Pamoja na kuwa, waangalizi wa uchaguzi hawakuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwa uchaguzi huo ufanyika siku chache kabla kutokana na changamoto zilizokuwepo.

Lakini kampeni zilisitishwa saa 24 kabla ya uchaguzi na uchaguzi huo baada ya kuhairishwa vyama vya siasa vilidhamiria kurudia kufanya kampeni tena.

Rais wa Muhammadu Buhari na mpinzani wake Atiku Abubakar walielezea kutoridhishwa kwao na hatua hiyo ya tume ya uchaguzi kusogeza mbele tarehe ya upigaji kura kwa madai ya kutokamiliaka kwa baadhi ya maandalizi muhimu.

Ambapo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Mahmood Yakubu, amedai kuwa kuchelewa kwa uchaguzi huo hakuhusiani na ushawishi wa kisiasa kwa namna yeyote.

Huku waaangalizi wa kimataifa katika uchaguzi mkuu uliosogezwa mbele nchini Nigeria wametoa wito kwa raia wa taifa hilo kuwa watulivu wakati maandalizi ya uchaguzi yanaendelea.