Tetesi za soka Ulaya Jumanne 19.02.2019: Sancho, Saiss, Berahino, Banega, Jovic, Diame

Kinda wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool huenda ikawasilisha ombi jingine la kinda wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho baada ya kumkosa alipokuwa katika klabu ya Manchester City. (Mirror)

Wolves wanakaribia kumpatia kiungo wa kati wa Morocco Romain Saiss mkataba mpya, 28. (Telegraph)

Arsenal itajaribu tena kumsaini kiungo wa kati wa Sevilla na Argentina Ever Banega, 30, mwisho wa msimu huu (Mirror)

Stoke itajaribu kumuuza mshambuliaji Saido Berahino muda tu dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu litakapofunguliwa baada ya mchezaji huyo wa Burundi kukamatwa kwa tuhuma za kunywa pombe na kuendesha gari. (Mail)

Barcelona wanapigiwa upatu kumsaini mshambuliaji wa Benfica Luka Jovic, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Eintracht Frankfurt. Real Madrid, Chelsea na Bayern Munich pia zinamnyatia kungo huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoka Serbia (Goal)

Mabingwa wa ligi ya Uhispania wanakamilisha usajili wa beki wa kati wa Brazil Vitao, 19, kutoka Palmeiras. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus wameiuliza Inter Milan kuhusu hatma ya Mauro Icardi lakini hawajaanza mazungumzo na mshambuliaji huyo wa Argentina ,25 ama ajenti wake. (Radio Rai via Four Four Two)

Kiungo wa kati wa Newcastle na Senegal Mo Diame, 31, anakaribia kuandikisha kandarasi mpya katika uwanja wa St James' Park. (Chronicle)

Kiungo wa kati wa Norway Martin Samuelsen, 21, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya VVV Venlo, anatarajiwa kurudi nyumbani kwao na klabu ya FK Haugesund. (Inside Futbol)

Kiungo wa kati wa West Brom na Uingereza Rekeem Harper, 18 anakaribia kutia saini kandarasi mpya (Express and Star)