Sheela-na-gigs: Michongo ya wanawake walio utupu inayopamba makanisa ya Uingereza

Haki miliki ya picha Sheela Na Gig project
Image caption sheela-na-gig katika eneo la Oaksey huko Wiltshire

Michongo ya wanawake yenye mamia ya miaka imekuwepo katika makanisa nchini Uingereza. Lakini ni nani aliyechonga picha hizo na kwa nini?

Mwaka 1992 na msanii mwandishi PJ harvey anacheza wimbo

Sheela-Na-Gig, ukiwa ndio wimbo wa pekee uliofanikiwa katika albamu yake iliokosolewa Dry.

Lakini hadi unapokuwa shabiki wa muziki wa karne ya 20 , ama mtaalamu wa usanifu katika kanisa la Norman, Kuna uwezekano mkubwa haujawahi kuusikia wimbo wa sheela-na-gig - ama hata umeusikia zaidi ya mara moja lakini hukuutambua.

Onyo: Picha hizi ni za utupu

Michongo hii ya wanawake iliofichwa inayowaonyesha wakishika seehemu zao za siri imezua hisia kali .

Haki miliki ya picha Sheela Na Gig project
Image caption Mchongo wa sheela-na-gigs" unaweza kupatikana katika kanisa la St Mary na St David huko Kilpeck, Herefordshire

Katika kipindi cha miaka 20 John Harding, kutoka kwa mradi wa Sheela Na Gig ametembea sana akitafuta michoro hiyo nchini humo.

Mapenzi yake na michoro hiyo yalianza pale alipotembelea kanisa moja mjini Shropshire 1998.

Baada ya kupata habari chache mitandaoni, aliamua kuchapisha kitu yeye mwenyewe akitarajia kwamba atapata habari zaidi.

Haipatikana sana: lakini pia sio jambo la kawaida, alisema. Unazipata mjini Shropshire ambapo zipo umbali wa maili 10 kila moja na ziko tofauti-lakini yote ni michoro ya wanawake walio utupu.

Taifa la Ireland lina idadi kubwa ya michongo hiyo huku nchini Uingereza ikiwa na michoro 60 na zaidi ikidaiwa kuonekana mara kwa mara , kulingana na bwana Harding.

Haki miliki ya picha Sheela Na Gig project
Image caption sheela-na-gig alipatikana akiwa ameweka uso wake chini katika kanisa la Llandrindod Wells

Lakini ni kwa nini michoro hii ya wanawake ilionyeshwa katika makanisa ya Uingereza, Ireland, Ufaransa na Uhispania, imezua hisa tofauti.

Wengine wanasema kuwa michoro hiyo inaadhimisha wakati ambao Ukristo ulikuwa haujakuja duniani , huku wengine wakisema kuwa ni ishara za wanawake walio na rutba ama hata ulinzi dhidi ya uovu.

Daktari Barbara Freitag , mwanzlishi wa Sheela-na-gigs: anaamini kwamba ilitengenezwa kwa makanisa kukuza kujifungua salama kwa wanawake

Haki miliki ya picha Getty Images/Steve Eichner
Image caption Mshindi wa tuzo ya Mercury Polly Jean Harvey drew inspiration alipendelea sheela-na-gig na kuimba wimbo mmoja

Lakini kwake Georgia Rhoades, mwanzilishi wa Decoding the Sheela-na-gig, anasema kuwa utupu huo unawakilishi 'mungu' wa duniani.

''Ilikuwa miungo ya kipagani inayotoa ishara ya mungu wa dunia anayetuzaa na kutuchukua wakati wa kifo'', aanaelezea.

Katika maeneo mengine , mabibi harusi walitakiwa kumshika Sheela kabla ya harusi hatua ambayo ilikuwa ikionyesha rutba aliokuwa nayo mungu huyo.

Hatahivyo anasema kuwa michongo hiyo ililenga kuwaonya watu dhidi ya madhambi ya tamaa.

Sheela katika taifa hili ni wanasesere walio na mvuto kwa jumla lakini nchini Ireland wengine wanatisha na huogofya tamaa ulionayo.

Haki miliki ya picha Sheela Na Gig project
Image caption sheela katika kanisa la at St Mary's Easthorpe, Colchester,

Nchini Uingereza picha za msichana Sheela na gigs zinaweza kupatikana katika kanisa la kipelk karibu na Hereford kulingana na bwana Harding.

Hatahivyo ni sheela aliyeko katika kanisa la Parish katika kijiji cha Wiltshire huko Oaksey, mwenye maziwa makubwa na sehemu zake nyeti zilizokubwa ambaye anampenda.

''Unapomuona Sheela wa Oaksey , wengi humtaja kuwa mungu mzuri'', anasema.

Mchoro huo uliopo mlangoni umewekewa paa ili kuulinda.

Haki miliki ya picha John Harding
Image caption Bwana John Harding

Lakini sio watu wote wanaopendelea michoro hii .

Katika kijiji cha Essex huko Eastrope, mchoro wa Sheela ulionekana kuwa mchafu na ulipelekwa katika makavazi baada ya kuwa katika bustani moja.

Michongo mingine imepatikana katika mito ikiwa na alama za kuchomeka, anasema bwana Harding, huku mingine ikitolewa , kuondolewa na hata kufichwa, kupakwa rangi nyekundu usoni na viongozi wa dini pamoja na waumini walioshangazwa.

Mwaka 2004, mchongo ulio utupu ambao ulikuwa katika kanisa huku Buncton , West Sussex miaka ya 11,000 ulishambuliwa licha ya kutokuwa na sehemu nyeti zilizokuwa zikionekana.

Haki miliki ya picha Brian Robert Marshall
Image caption Watu wanapomuona sheela katika eneo la Oaksey husema ni mungu mzuri

Kwa picha michoro ya Sheela-n gigs

Haki miliki ya picha Sheela Na Gig project
Image caption Sheela wawili
Haki miliki ya picha Sheela Na Gig project
Image caption Sheela katika paa la kanisa la Avening Church huko Gloucestershire
Haki miliki ya picha Sheela Na Gig project
Image caption sheela anaonekana akiwa utupu latika eneo la Whittlesford, Cambridgeshire

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii