Wanasayansi wanasema baadhi ya gesi inayosababisha uchafuzi wa mazingira hutokana na shughuli za kilimo kama vile ufugaji

lab grown meat

Chanzo cha picha, Getty Images

Ukuzaji wa nyama katika maabara badala ya ulaji wa nyama halisi huenda ikawa na madhara kwa mazingira siku zijazo.

Watafiti wanatafuta njia mbadala ya ukuzaji nyama badala ya ulaji nyama unaotokana na wanyama wanaofugwa kwasababu ufugaji unachangia kupanga kwa viwango vya joto duniani.

Hata hivyo nyama inayokuzwa kwenye maabara huenda ikawa ndio suluhisho japo wanahoji aina ya kawi (nishati) itakayotumiwa kukuza nyama hiyo.

Kwanini wanasayansi wanajaribu kukuza nyama kwenye maabara?

Kumekuwa na hofu kuhusiana na madhara ya ulaji nyama kwa mazingira.

Karibu robo ya gesi chafu inayosababisha uchafuzi wa mazingira hutokana na shughuli za kilimo kama vile ufugaji.

Inasadikiwa kuwa mbolea inayotokana na samadi ya mifugo kama vile methane na nitrous oxide huchangia uchafuzi wa mazingira.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Samadi ya mifugo inatoa gesi kama vile methane na nitrous oxide ambayo huchangia uchafuzi wa mazingira

Juhudi za kukuza nyama katika maabara zimefikia wapi?

Mwaka 2013 kundi la wanasayansi kutoka nchini Ujerumani lilidai kukuza nyama kwa mara ua kwanza katika maabara kwa kutumia njia ya kisayansi.

Tangu wakati huo kumekuwa na gumzo kuhusiana na njia hiyo ya ukuzaji nyama kama njia ya kusitisha uchinjaji wa wanyama na kuhifadhi mazingira

Hatua kubwa imepigwa katika mpango huo hasa katika baadhi ya makampuni mjini California.

Mwaka jana, Kampuni moja ya chakula mjini San Francisco ilivumbua mfumo wa kukuza nyama ya kuku katika maabara kutokana na seli ya unyoya wa kuku.

Ladha ya nyama hiyo-ni sawa na ile ya kuku wa kawaida,tofauti ni kuwa imekuzwa kitaalamu katika maabara kutokana na seli ya mnyama.

Tyson Foods, moja ya kampuni kubwa ya nyama nchini Marekani imewekeza katika njia ya kisayansi ya ukuzaji nyama.

Maelezo ya picha,

Nyama ya kuku iliyotengenezwa katika maabara

Kampuni nyingine inayojishughulisha na uuzaji wa nya imesema "ni bora kuwekeza kwa ukuzaji wa nyama katika maabara badala ya kufuga wanyama".

Licha ya hatua hizo hakujashuhudiwa kiwango kikubwa cha ukuzaji wa nyama kwa njia ya kisayansi katika maabara.

Nyama inayokuzwa katika maabara ina faida yoyote?

Wanasayansi wanasema masuala kama uchafuzi wa mazingira ikiwa ni papoja na maji hayajitokezi katiaka mfumo wa ukuzaji nyama kisayansi.

Lakini wataalamu wengine wanasema hilo bado lina mjadala.

"Nyama hiyo pia huenda ikawa na kamikali ambayo inahitaji maji mengi kusafishwa" anasema Prof Jean-Francois Hocquette, kutoka taasisi ya kitaifa ya utafiti wa kilimo nchini Ufaransa ambaye hakuhusika na utafiti huu wa sasa.

Utafiti utawaogopesha watu kula nyama ya maabara?

Ni mapema kuangazia hilo kwasababu bado ulaji wa nyama hiyo haujaidhinishwa.

Baadhi ya watafiti wanasema changamoto kubwa kwa wanasayansi ni kuwahakikishia walaji nyama kwamba nyama hiyo ya maaabara haina madhara ya kiafya.

"Ifahamike kuwa watu wengi hawana habari kuhusu nyama iliyokuzwa katika maabara, na madhara ya ufugaji kwa mazingira,"anasema, Dr Chris Bryant kutoka chuo kikuu cha Bath ambaye amesomea suala hilo.

Mjadala kuhusiana na nyama inayokuzwa kupitia njia ya kisayansi ikiendelea kushika kasi, baadhi ya wafugaji wanahoji jinsi bidhaa hiyo itakavyo uzwa- Je ni nyama safi, nyama bila myama kuchinjwa, protini safi au nyama ya kawaida tu.