Jinsi wanaume waliyo na uhusiano wa kando wanavyohusishwa na maandamano Sudan

Women protesting in Khartoum, Sudan

Chanzo cha picha, Reuters

Katika msururu wa barua kutoka kwa wanahabari wa Afrika, Zeinab Mohammed Salih anaangazia jinsi wanawake nchini Sudan wanavyotumia mtandao wa kijamii wa Facebook kufichua madai ya unyanyasaji wanayopitia mikononi mwa waume zao huku maandamano dhidi ya serikali yakiendelea.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa wanawake kadhaa walijiunga na maandamano ya kitaifa ya kila siku ambayo yalianza katikati ya mwezi Disemba mwaka jana.

Licha ya msako mkali unaofanywa na maafisa wa usalama na ripoti ya visa vya unyanyasaji watu nchini Sudan wameendelea kushiriki maandamano hayo.

Zaidi ya watu 50 wanadhaniwa kufariki mikononi mwa maafisa wa usalama na wengine wengi kuteswa, makundi ya kutetea haki yanasema .

70% ya wanawake wamejitokeza katika baadhi ya maandamano hayo, waangalizi wanasema, hali ambayo inaashiria uasi dhidi ya sheria za kikoloni katika taifa hilo la kiislam.

Wote wanafunika vichwa vyao wa sheria ya nchi ambayo inadhibiti mavazi yao - tkwa mfano wanaweza kuadhibiwa kwa kuvalia nguo kama vile suruale ya miguu mirefu ambayo inachukuliwa kuwa nguo isiyokuwa ya heshima.

Lakini mwanafunzi mmoja alimueleza mwanahabari wetu jinsi maafisa wa usalama walivyomvua hijab wakati alipokamatwa Januari 31 katika mji mkuu wa Khartoum.

"Walirarua hijab yangu kichwani kwa kutumia wembe na kutishia kunibaka waliponipeleka katika eneo la viungani mwa Khartoum," Jode Tariq alisema.

Maelezo ya video,

Je ni nini kinafanyika ndain ya vizuizi vya siri Sudan?

Mwanamke mwingine wa miaka 24 pia aliasimulia kisa kama hicho mikononi mwa maafisa wa usalama mapema mwezi Januari.

"Walininyoa nywele mimi na mwanamke mwingine katika eneo ambalo hatukujua ni wapi lakini ilikua kituo cha kuzuilia watu," alisema Afraa Turky.

Wanahabari wa kike Shamael al-Nnoor na Durra Gambo, ambao pia walikamatwa kwa kuangazia maandamano hayo mwezi uliyopita wanasema baadhi ya wanawake waliyokutana nao kizuizini waliwaambia kuwa walinyanyaswa kingono na maafisa wa usalama.

Hatima ya wanawake wengi waliyofungwa gerezani haijulikani tangu walipokamatwaha na kuzuiliwa.

Sheria ya utangamano wa umma nchini Sudan

  • Kifungu cha 152 cha sheria kinaangazi "vitendo vya kudhalilisha" katika maeneo ya ummain.
  • Hii inajumuisha kuvalia nguo "isiyokuwa ya heshima" au "ambayo inaweza kuamsha hisi za watu"
  • Wanawake lazima wavae hijab na hawaruhusiwi kuvaa suruali ya miguu mirefu.
  • Kati ya wanawake 40,000 na 50,000 wanakamatwa na kuadhibiwa na polisi kwa kukiuka sheria ya mavazi.
  • Wanawake pia wameadhibiwa chini ya sheria hii kwa kuwa peke yao na wanaume.
  • Watu pia wanaweza kushtakiwa chini ya sheria hii kwa kunywa pombe.

Lakini wanawake sasa wanapinga madai ya unyanyasaji dhidi yao kwa kutumia kundi moja la wanachama wanawake pekee katika mtando wa Facebook.

Ukurasa huo ulibuniwa miaka mitatu iliyopita kuwatambua waume waliyo na uhusiano wa kando na kuwafuatilia wapenzi wao.

Maafisa wa ujesusi kutoka shirika la kitaifa la ujasusi la Sudan wamehusishwa na visa vya kutumia nguvu kuvunja maandamano yaliyoanza katika mji wa mashariki wa Atbara kupinga ongezeko la bei ya mkate.

Waandamanaji sasa wanapiga picha watu wanoshikiwa kuwa maajenti wa upelelezi katika maandamano hayo na kusambazwa kwatika ukurasa huo wa Facebook, unaofahamika kama Minbar-Shat, ambayo kwa lugha ya kiarabu ya Sudan inamaanisha "Mapenzi kupita kiasi".

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Waandamanaji wanalalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na wanataka rais Bashir kuondoka madarakani

'Usinaingalie'

Mamlaka nchini Sudan zimejaribu kufunga mitandao ya kijamii, lakini wanawake hao wamefanikiwa kutumia mfumo mbadala wa unaofahamika kama Virtual Private Networks (VPN), ambao unauwezo wa kuficha sehemu alipo mtumiaji wa mtandao.

Mbinu hiyo ya kuwafichua maajenti wa ujasusi imefanikiwa kiasi cha kuwafanya maajenti hao kuficha nyuso zao kwa hofu ya kutambuliwa na kutengwa na jamii.

Baadhi ya waandamanaji waliiambia BBC kuwa walipokamatwa walilazimika kuangalia chini kwa saa kadhaa.

Mmoja wao alisema, "Niligongwa kwa mti kichwani kwasababu niliangalia upande kimakosa, 'Unataka kunipiga picha kisha utume katika kundi la Minbar-Shat? Usiniangalie.'"

Waandamanaji pia wanaficha nyuso zao lakini kwasababu ya kujikinga na mabomu ya kutoa machozi.

Minbar-Shat sasa inatumia ukurasa wa Toyota wa Facebook kuwafahamisha kuwa gari zao zinatumiwa na maafisa wa ujasusi wa Sudan, NISS, kuwakamata waandamanaji na mara nyingine kuwagonga kimakusudi.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wandamanaji wengi hufunika nyuso zao kujikinga na mabomu ya machozi

Kuna haja ya kufanyia marekebisho sheria ya mavazi?

Sudan ina rekodi mbaya inapokuja suala la kudumisha haki za wanawake, shirika la kuttetea haki la Human Rights Watch linasema maafisa wa usalama mara nyingi wamekuwa wakitumia vurugu kuwanyamazisha wanawake.

Siku kumi zilizopita kundi la wanawake lilibakwa na wanamgambo wa serikali katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dafur kaskazini ambako Umoja wa mataifa unasema ubakaji umetumiwa kama silaha ya vita wakati wa mapigano miaka 13 iliyopita.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Rais Bashir,ameingoza Sudan kwa karibu miaka 30

Maandamano ya kuipinga serikali kwa mara ya kwanza yalianza katikati mwa mwezi Desemba mwaka jana kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha.

Bei ya mkate ilipanda mara tatu katika baadhi ya maeneo na bei ya mafuta pia ikapanda.

Bi Tariq na Ms Turky, ambao walinyolewa nywele na maajenti wa ujesusi mwezi uliyopita wanasisitiza kuwa wataendelea kuandamana hadi Bw. Mr Bashir atakapong'atuka madarakani.