Mbunifu mahiri wa mavazi afariki akiwa na umri wa miaka 85

Lagerfeld posing with a painting of his cat

Chanzo cha picha, AFP

Mbunifu maarufu duniani Karl Lagerfeld, afariki dunia mjini Paris mara baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mbunifu huyo mwenye asili ya Ujerumani alikuwa mkurugenzi katika kampuni ya Chanel na Fendi , kampuni ambayo ina sifa kubwa katika sekta ya mitindo duniani .

Saini yake ya nywele zilizofungwa nyuma pamoja na miwani meusi zilimfanya ajulikane zaidi duniani kote.

Wabuni wakubwa katika sekta hiyo akiwemo mbunifu kutoka Italia Donatella Versace ametuma salamu zake za rambirambi.

Tovuti yake Lagerfeld, umeandika kuwa alizaliwa mwaka 1938 - Ingawa katika majarida mengine wameongeza miaka mitano ya umri wake.

Tetesi za kuugua kwa Lagerfeld zilisikika wiki chache baada ya kuanza kutoonekana katika matukio kadhaa likiwemo onesho la kiangazi la Chanel lililofanyika mwezi uliopita.

Mwanamtindo huyo alifariki majira ya asubuhi baada ya kulazwa hospitalini kwa usiku mmoja, ripoti za Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeandika.

Akiwa ni mbunifu ambaye alileta mabadiliko makubwa katika kampuni ya Chanel, ambayo jina lake lilikuwa kutokana na uhodari wa kazi yake .

Ukiachilia mbali kazi yake ya ubunifu, Lagerfeld aliwahi kuandikwa katika vichwa habari mara kadhaa katika masuala ya uchochezi na hata kauli ambazo zilikuwa zinakera.

Salamu za rambirambi?

Maelezo ya picha,

Muonekano uliokuwa unamtambulisha katika ubunifu

Wadau wa sekta ya mitindo wameandika mengi kumsifu Lagerfeld kwa umahiri wa kazi yake.

Donatella Versace alisema kuwa mbunifu huyo alikuwa mtu mwerevu sana na aligusa maisha ya watu wengi na alikuwa chanzo cha yeye pamoja na marehemu kaka yake kuvutiwa na kazi hii ya ubunifu.

Wintour ilimuelezea mbunifu huyo kuwa na alikuwa na akili sana kama kuvuta pumzi.

"Karl alikuwa mcheshi na mkarimu kupita maelezo,Nitamkumbuka sana"

Mwanamitindo, Claudia Schiffer, alisema: " Kile ambacho Karl alifanya ni sanaa ambayo haiwezi kuzibwa na mtu mwingine. Yeye pekee ndio aliweza kufanya nguo za rangi nyeusi na nyeupe kupendeza."

Mmiliki wa Chanel , Alain Wertheimer alianza kumpa sifa Lagerfeld kwa mabadiliko aliyoyaleta katika mitindo tangu mwaka 1983.

"Shukrani za dhati kwa mbunifu wa kipekee aliyekuwa ana akili sana, Karl Lagerfeld kwa muda wote aliotumikia Chanel duniani kote", alieleza.

Watu maarufu wametuma salamu zao za rambirambi akiwemo Victoria Beckham, mcheza filamu Diane Kruger na wanamitindo Gigi pamoja na Bella Hadid.

Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump aliweka picha ya mwanamtindo huyo katika kurasa yake ya Twitter.

Maisha yake katika mitindo

Karl Otto Lagerfeldt alizaliwa kabla ya vita kutokea Ujerumani miaka ya 1930.

Lagerfeld alibadilisha jina lake kutoka Lagerfeldt, kwa sababu aliamini lilikuwa linavutia katika biashara zaidi.

Alihamia Paris akiwa kijana mdogo, na akawa msaidizi wa mbunifu Pierre Balmain kabla hajaanza kufanya kazi na Fendi pamoja na Chloe katika miaka ya 1960.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lagerfeld mwaka 1979

Lakini mbunifu huyo alijulikana zaidi katika lebo ya Chanel.

Alianza kazi yake ya mitindo katika kiwanda cha Chanel mwaka 1983, muongo mmoja baada ya Coco Chanel kufariki.

Ubunifu wa Lagerfeld uliweza kurudisha uhai wa lebo hiyo ya Chanel .

Aliweza pia kushirikiana na wabunifu wa H&M - kabla jina hilo halijapata umaarufu mkubwa.

Lagerfeld alijulikana pia kwa kuibua vipaji vipya vya wabunifu wa mitindo kama kipaji cha Victoria Beckham - ambaye alimsifu kwa ukarimu wake.

Lagerfeld alichelewa kupata umaarufu wake, mpaka alipokuwa ana umri mkubwa kipindi ambacho alianza kuvaa miwani meusi na suti nyeusi pamoja na kuandika saini ya nywele zilizofungwa kwa nyuma pamoja na miwani meusi.

Lagerfeld alizungumzia mara kadhaa kuhusu kupenda muonekano wake.

Licha ya umri wake kuwa mkubwa, sekta ya ubunifu iliendelea kuthamini kazi yake, Na alionekana kuendelea kupata sifa za umahiri wake alipoonekana kubuni kwa ajili ya Kim Kardashian mwaka 2015.