Boniface Murage: Mtu aliyejaribu kuitorosha familia yake hospitali kuu ya Kenyatta kwa kushindwa kulipa gharama aachiliwa huru Kenya

Bwana Boniface Murage kulia mkewe Agnes Elewo na mwanao aliyeleta furaha katika familia hiyo

Tarehe 16, mwezi Februari ,2019 itaendelea kusalia katika kumbukumbu za Boniface Murage na mkewe Agnes Elewo.

Bi Elewo alilazwa katika hospitali kuu ya Kenyatta jijini Nairobi (KNH) pamoja na mtoto wao wa mwezi mmoja ambaye alikuwa mgonjwa.

Alikuwa na vipimo vya juu vya joto mwilini pamoja na tatizo la kupumua.

Bwana Murage alijawa na wasiwasi na hakuweza kufikiria kwamba mkewe mpendwa na mwanawe wa kike walikuwa wanazuiliwa katika hospitali ya umma kwasababu ya kukosa kushindwa kulipa gharama ya kulazwa

''Mimi hufanya kazi ya mkono, na hutengeneza kama dola tano kwa siku ama saa nyengine ninakosa kabisa, '', alisema Murage

Jamaa huyo ambaye kama kawaida humtembelea mkewe kila siku akimpelekea chakula alimshawishi kuhusu njama ya kutoroka katika hospitali ya KNH ili kukwepa kulipa gharama ya hospitali ksh.56,937 walizokuwa wakidaiwa.

''Nilijaribu kuchangisha fedha lakini nikaona kwamba kila ninapoendelea kuchangisha fedha ndipo gharama inapozidi'', aliongezea.

Maelezo ya video,

Aliyejaribu kumtorosha mwanawe mchanga hospitalini aachiliwa huru

Mtoto huyo alilazwa mnamo tarehe 26 mwezi Januari na alitarajiwa kutolewa tarehe 11 mwezi Februari.

Lakini kwa kuwa mkuu wa familia hiyo hakujuwa vile atakavyolipa gharama hiyo ya kulazwa ambayo ilikuwa ksh.46,000, mama na mtoto wake walisalia katika kituo hicho cha afya kwa wiki moja zaidi.

Marafiki wa bwana Murage, majirani, na wafanyikazi wenzake wanaochimba mahandaki walifanikiwa kuchangisha ksh, 2,000, ikiwa ni kiwango cha chini sana cha fedha zilizokuwa zikihitajika.

Kwa takriban siku 21, alimtembelea mkewe na mwanawe, akiwapelekea uji kama chakula cha kila siku.

Na baadaye akapata wazo hili: Kwa nini nisimuweke mtoto ndani ya begi na kuondoka katika hospitali hiyo.? Hakuna mtu angegundua.

''Nilienda hospitali ya Kenyatta nikapata kwamba mtoto amelala, hata sikuona kitu chengine ningemwambia mke wangu. Nilimuuliza Wangechi anaweza kutosha hapa? Akaniambia ndio anaweza kutosha ndani ya begi nililokuwa nimebeba, nikamwambia tumuweke ndani yake akiwa amelala twende nyumbani''.

Maelezo ya picha,

Kulingana na Murage aliwaambia maafisa hao ukweli na hata hakimu wa mahakama ambayo alikuwa amewasilishwa siku ya Jumatatu.

Akijuwa matatizo ya kifedha ya mumewe, bi Elewo hakukataa pendekezo la mumewe.

Baadaye Murage alibeba begi hilo ambalo aliweka tundu ili kumzuia mtoto huyo kukosa hewa na mkewe akamfuata nyuma.

Bwana Murage hakutarajia kusimamishwa na mtu yeyote, lakini kwa ghafla aksimamishwa.

Alikataa kwa muda lakini walinzi hao walipotaka begi hilo kufunguliwa, maafisa wa polisi waliitwa mara moja kwa kua waliamini alikuwa na njama za kumuua mtoto huyo.

''Nikitoka nilisimamishwa na mlinzi akaniuliza ni nini nilichokuwa nimebeba nikasema ni vyombo vya kubebea chakula, akasema hebu nione ndiposa akapata mtoto, nikachukua mtoto wangu na kumwambia nimeshindwa na uwezo wa kulipa gharama ya hospitali'', alisema Murage.

Huku Murage akichukuliwa na maafisa hao wa polisi na kufungiwa katika seli, mkewe alisalia amezuiliwa katika hospitali hiyo.

Kulingana na Murage aliwaambia maafisa hao ukweli na hata hakimu wa mahakama ambayo alikuwa amewasilishwa siku ya Jumatatu.

''Kwa kweli sikujua ni wapi kwengine ningetafuta usaidizi, nilikuwa nimeshindwa na niliamua kuomba kwamba njama hiyo ya kutoroka hospitalini ingefanya kazi'', alisema.

Maelezo ya picha,

Wanandoa hao wameoana kwa mwaka mmoja na miezi sita.

Alipowasilishwa mbele ya hakimu mkuu mkazi Caroline Nzibe, siku ya Jumanne, hakujua kwamba mkewe alikuwa amewachiliwa na gharama hiyo ya kulazwa kulipwa na kwamba angekuwa huru kupatiwa kazi na kuwa tajiri kiasi.

Alikuwa amekiri kujaribu kufanya makosa.

Alipoulizwa iwapo angethubutu kufanya makosa kama hayo tena, licha ya kupewa kifungo cha nyumbani cha miezi mitatu na hakimu Nzibe alikiri na kusema kuwa yeye sio muhalifu.

Wanandoa hao wameoana kwa mwaka mmoja na miezi sita.

Murage anasema kuwa angependelea kumsomesha mwanaye ili kuwa daktari kwa lengo la kuwasaidia wengine ambao wapo katika hospitali hiyo ya Kenyatta.

Wanandoa hao wana umri wa miaka 22 na wanaishi katika chumba chao kimoja katika eneo la Ole Kasasi eneo la Ongata Rongai.