Boniface Murage: Aliyejaribu kumtorosha mwanawe mchanga hospitalini aachiliwa huru

Boniface Murage: Aliyejaribu kumtorosha mwanawe mchanga hospitalini aachiliwa huru

Mtu aliyejaribu kuitorosha familia yake hospitali kuu ya Kenyatta kwa kushindwa kulipa gharama aachiliwa huru Kenya.

arehe 16, mwezi Februari ,2019 itaendelea kusalia katika kumbukumbu za Boniface Murage na mkewe Agnes Elewo.

Bi Elewo alilazwa katika hospitali kuu ya Kenyatta jijini Nairobi (KNH) pamoja na mtoto wao wa mwezi mmoja ambaye alikuwa mgonjwa.