Wazazi waliyo na watoto walemavu Zanzibar washauriwa kutowaficha majumbani

Wazazi waliyo na watoto walemavu Zanzibar washauriwa kutowaficha majumbani

Jumla ya watoto 22 wenye ulemavu wa macho visiwani Zanzibar wameibuliwa na kuandikishwa shule katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.Watoto hao wametoka katika wilaya tatu visiwani humo, ikiwa ni jitihada za kutafuta watoto waliofichwa kutokana na matatizo ya uoni hafifu ili kuwapa fursa adhim ya kuandikishwa shule. Mwandishi wa BBC Halima Nyanza amezungumza na Adili Mohammed Ali Mratibu wa Jumuia ya Wasioona Zanzibar.