Tuzo za Brit 2019: Beyonce na Jay-Z 'wanavutiwa na Meghan Markle

Image of Beyonce and Jay-Z in front of a portrait of Meghan Markle

Chanzo cha picha, Beyonce/Instagram

Beyonce na Jay-Z wakiwa wamepiga picha mbele ya picha ya mwana mfalme akiwa amevalia taji wakati wakiwa wamekubali kuwa kundi la zuri kimataifa katika tuzo ya Brits.

Beyonce aliandika katika kurasa yake ya Facebook na kusema kuwa kwa heshima ya kihistoria ya watu weusi, tunatoa heshima kwa moja ya picha ambayo inatuwakilisha."

Picha kama hiyo pia wanaifananisha na picha ya video ambayo walipiga wakiwa wamesimama mbele ya picha maarufu ya Monalisa huko Louvre, Paris.

Lakini katika tuzo za Brits, Wapenzi hao walipiga picha karibu na picha ya Meghan Markle.

Beyonce aliongeza kusema: "Hongera kwa kuwa mjamzito, tunakutakia furaha tele."

Katika gazeti la Guardian, muhariri wa muziki Laura Snapes amesema uamuzi wa kukubali kupata tuzo yao mbele ya picha ya Meghan ilikuwa ni jambo zuri sana.

"Ilivutia sana na hii ni ishara ya kumuunga mkono mwanamke mweusi ambaye ameolewa na mwana mfalme wa Uingereza.

Watu wengine walipendekeza kwamba picha ya Beyonce na Jay Z ilikuwa ni ujumbe kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kumuunga mkono Meghan.

'Hawakuambiwa kufanya hivyo ,waliamua tu wenyewe kupiga picha hiyo'

Msanii aliyepiga picha ya Meghan , Tim O'Brien, alisema kwenye redio kuwa Meghan anaibadili taswira ya Uingereza na amekuwa ishara kuwa utawala wa watu weupe upo katika maendeo yote duniani.

Lakini anatuambia kuwa alibaini kuwa Beyonce na Jay Z ametumia mfano wa picha aliyomchora Meghan kama watu wengine tu walivyoona.

"Sikutaarifiwa, niliona tu kwenye mtandao wa kijamii.Yan kwa saa 24 imekuwa ikivutia." mpiga picha hiyo aeleza.

Mchoro huu uliagizwa kuchorwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 kwa ajili ya jarida linaloitwa 'The key'.

Chanzo cha picha, Tim O'Brien

Mpiga picha huyo bado hana uhakika kama atawaambia watayarishaji wa tuzo za Brit kuwaambia wasanii hao wapenzi kulipia picha yake walioitumia.

Lakini mpaka sasa picha hiyo imekuwa ikinunuliwa sana mtandaoni , jambo ambalo linaridhisha.

Tim aliongeza kusema kuwa picha asili ya mchoro huo inauzwa hivyo kama Beyonce na Jay Z wanataka kuinunua , wanakaribishwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

"Kama utachora watu wema , watu watasema kuwa picha ni nzuri na zinavutia, aeleza mchoraji wa picha ya mwana mfalme

Mwanafalme Prince Harry alimuoa Meghan mwaka jana, na wamekuwa kwenye vichwa vya habari mwaka huu na jana .

Baadhi ya watu wamekuwa wakilaumu sehemu ya vyombo vya habari vimekuwa vikimripoti Meghan kwa mambo ambayo sio mazuri- wakati Meghan sasa akiwa na ujauzito wa miezi saba.