Godfrey Kasaya: Alazimika kula mboga za kiasili baada ya kupatwa na maradhi

Godfrey Kasaya: Alazimika kula mboga za kiasili baada ya kupatwa na maradhi

Mtindo wa maisha siku hizi umewafanya wengi kukosa kupata lishe inayosaidia afya zao. Watu wengi hasa katika maeneo ya mjini wamekua wakipata vyakula vilivyopakiwa kutoka dukani, migahawa na maduka ya jumla. Vyakula hivi vingi vimelaumiwa kusababisha magonjwa yanayotokana na mtindo wa maisha uliowafanya wengi kukosa kupata lishe inayosaidia afya zao. Godfrey Kasaya kutoka Kenya amelazimika kuanza kula mboga ya kiasili baada ya kupatwa na maradhi ya msukumo wa damu.