Wanaharakati wa kuhifadhi wanyama wameikosoa Botswana kuhusu marufuku ya uwindaji tembo

Botswana inajivunia kuwa na thuluthi tatu ya tembo barani Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Botswana inajivunia kuwa na thuluthi tatu ya tembo barani Afrika

Ripoti ya mawaziri nchini Botswana inapendekeza kuondolewa kwa marufuku ya miaka minne iliyopita ili kupunguza idadi ya tembo nchini humo.

Baada ya miezi kadhaa ya mashauriano ya umma na wanachama wa kamati ya mawaziri, wamependekeza kububuniwe mbini ya kupunguza idadi ya tembo.

Botswana inakadiriwa kuwa na tembo karibu 130,000, japo kuna wale wanahoji kuwa idadi hiyo ni kubwa sana mazingira hasa ikizingatiwa ongezeko la mzozo kati ya wanyama na binadamu.

Lakini wengine wanasema sekta ya utalii nchini humo imekuwa tangu marufuku dhidi ya wanyama hao ilipowekwa na kuongeza kuwa hatua hiyo huenda ikaathiri juhudi ya kimataifa ya uhifadhi wa wanyama hao.

Muda mfupi baada ya kuingia madarakani mwezi April mwaka 2018, rais Mokgweetsi Masisi aliwaagiza mawaziri kuchunguza upya marufuku ya uwindaji iliyokuwa imewekwa na mtangulizi wake Ian Khama mwaka 2014.

Mikutano ya umma wa kujadili suala hilo ilijumuisha mashirika ya kiraia, jamii na watu binafi.

Riopoti hiyo inapendekeza:

  • Kuondolewa kwa marufuku ya uwindaji
  • Idadi ya tembo nchini humo kudhibitiwa
  • Kufungwa kwa njia zinazotumiwa na wanyama kuhama kutoka eneo moja hadi nyingine kwasababu"hazisaidii za uhifadhi wa wanyama wa taifa hilo"
  • Kuwekwa kwa mipaka ya mbuga za wanyama ili kukabiliana na "mzozo kati ya wanyama na binadamu"

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais Masisi amepokea ripoti hiyo ambayo itapigwa msasa baada ya mashauriano zaidi kabla ya kuanza kutekelezwa.

"Naahidi taifa kuwa tutazingatia ripoti hii." alisema.

"Ikiwezekana tutalipatia bunge fursa ya kujadili ripoti hii kabla kuidhinishwa kwake."

Kwanini mzozo kati ya binnadamu na tembo inazidi kuongezeka?

Utafiti unaonesha kuwa tembo wanasafiri mbali na umbali wa safari zao umeendelea kuongezeka.

Mkurugenzai wa kitenngo cha wanyamapori katika hifadhi ya kitaifa ya wanyama, Otisitwe Tiroyamodimo, anasema kuna sababu nyingi ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Tembo wanaweza kusababisha uharibifu mkubwa wanapovamia mashamba na wakati mwingine wanaweza kuua watu wakijaribu kuwafukuza.

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wanazungumziaje pendekezo la kuondoa marufuku ya uwindaji tembo?

Wale ambao walipoteza ajira zao baada ya marufuku ya uwindaji kuwekwa wanasema wataunga mkono mabadiliko hayo.

Lakini wanaharakati wa kuhifadhi wanyamapori wanapinga vikali wazo la kupunguza idadi ya tembo, na kuongeza kuwa hatua ya kuwapunguza au kuwawinda itaathiri utalii wa kimataifa.

Utalii ni chanzo cha pili cha pili cha Botswana cha kipato cha kigeni baada ya madini ya almasi.

Huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mwezi Oktoba mwaka huu, serikali imejipata katika njia panda.

Je iondoe marufuku ya uwindaji haramu wa tembo ili kujipatia kura za watu wa vijijini ama idumishe marufuki hiyo ili iendelee kujizolea sifa ya kuwa taifa linaowavutia watalii kutokana na tembo wake?